
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo, Alban Kihulla
WAKALA wa Vipimo (WMA) imesema kuwa kati ya mafanikio makubwa na ya kihistoria kwa miaka 4 ya Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassani tangu kuwepo kwa wakala hiyo ni kupata ajira za wafanyakazi wapatao 186 jambo ambalo halijawahi kutokea toka Tanganyika kupata uhuru. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).
Hayo yameelezwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo, Alban Kihulla alipokuwa akitoa taarifa ya mafanikio kwa kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Serikali iliyopo Madarakani katika Ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO Jijini Dodoma.
Kihulla amesema kuwa katika historia ya kuwepo Wakala wa Vipimo haijawahi kuwa na watumishi wa kutosha kama ilivyo idadi ya sasa jambo ambalo litasaidia walaka hiyo kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa.
“Katika mafanikio makubwa ambayo Wakala wa Vipimo inaweza kujivunia kwa kipindi cha miaka 4 ni kufanikiwa kuwaajiri watumishi 186 ambapo 150 wameisha kuwa na ajira kamili na 36 wapo katika hatua za usahili.
“Tangu kuanzishwa wakala hiyo ilikuwa na changamoto ya kukosa watumishi jambo ambalo lilikuwa likifanya utendaji kazi kuwa mgumu kidogo tofauti na utendaji wa sasa ambapo watumishi wameongezeka,” amesema Kihula.
Ili kudhibitisha hilo Kihula amesema kuwa historia ya Idara ya Vipimo nchini Tanzania inaanza mwaka 1884 hadi 1918 wakati wa utawala wa Kijerumani.
Amesema kuwa wakati huo, Idara ya Vipimo ilikuwa chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani na iliendeshwa na Kamishna wa Polisi.
Ameeleza kuwa baada ya kipindi hicho, kuanzia mwaka 1919 hadi 1962, wakati wa utawala wa Kiingereza, Idara ya Vipimo iliendelea kubakia chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani, kiongozi wake akiwa na cheo cha Kamishna wa Polisi.
Ameeleza baada ya kupata uhuru, kuanzia mwaka 1961 hadi tarehe 16 Mei 2002, Idara ya Vipimo ilikuwa chini Wizara ya Viwanda na Biashara baada ya kuonekana shughuli zake zinaendana na biashara.
Amesema kuwa mnamo tarehe 17 Mei 2002, Idara hiyo ya Vipimo ilipandishwa hadhi na kuanzishwa rasmi kuwa Wakala wa Vipimo, na imeendelea kufanya kazi kwa mfumo huo hadi sasa.
Aidha Kihulla akifafanua mafanikio kwa kipindi cha miaka minne (4) kupatikana kwa ajira za Maafisa wapya wa ukaguzi wa Vipimo.
“Utekelezaji wa majukumu ya kila siku ya Wakala wa Vipimo unahitaji nguvu kazi ya rasilimali watu ambao watafanya ukaguzi na uhakiki wa vipimo.
Wakala inaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuiwezesha kupata ajira za watumishi 186 wa kada ya ukaguzi wa vipimo ambao wataongeza nguvu kwenye jukumu la uhakiki na ukaguzi wa vipimo hapa nchini.
Amesema kuwa kwa mwaka 2021/2022 watumishi walikuwa 2 mwaka 2022/23 watumishi walikuwa 7,mwaka 2023/2024,watumishi walikuwa 17 na mwaka 2024/2025 watumishi ni 186.
Pamoja na Mafanikio hayo ya kihistoria Kihulla amewahimiza watanzania kutopenda kununua vitu bila kujali vipimo vinavyotambuliwa kisheria.
Mfano amewashauri wajenzi kitonunua magati ya mchanga au kokoto kwa idadi ya magari bali wazingatie ujazo wa gari sambamba na wale wote wanaouza gesi hasilia ya kutumia majumbani kutumia mizani ya kupimia mitungi ya gesi.
ZINAZOFANANA
TCI yafungua ofisi Njombe, kuleta huduma za uwekezaji karibu
NEMC kupambana na magugu maji Ziwa Victoria
Chadema kuwafungulia kesi Makalla, Gazeti la Habari Leo