March 26, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

NEMC kupambana na magugu maji Ziwa Victoria

 

BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), limesema kuwa limejipanga kuhakikisha linavuna magugu maji maji mapya katika ziwa Victoria. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkui wa NEMC,Dk. Sware Semesi alipokuwa akitoa taarifa ya mafanikio ya miaka 4 ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hasani kwa waandishi wa habari katika ukumbiwa wa Idara ya Habari-MAELEZO Jijini Dodoma.

Akizungumzia umuhimu wa ziwa hilo Dk. Semesi amesema NEMC kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa mazingira kwa kushirikiana na nchi jirani ambazo zinapakana na Ziwa Victoria wamafanya kila juhudi ili kuokoa ziwa hilo kutokana na kuibuka magugu maji mapya ambayo yanaweza kusababisha changamoto mbalimbali katika ziwa hilo.

Akitaja baadhi ya changamoto ambazo zinaweza kujitokeza kama magugu maji hayatavunwa ni pale ambapo yataitesa miundombinu katika ziwa hilo ikiwa ni kusababosha vivuko kuongiliwa na kukwamishaji uwekezaji mkubwa katika ziwa hilo.

Akiendelea kuzungumzia mafanikio kwa kipindi cha miaka hiyo minne, ameaema kuwa kwa miaka minne ya 2020/21-2024/25, limeendelea kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na kufikia zaidi ya asilimia 68 ya malengo yaliyowekwa.

Akiyataja malengo hayo amesema lengo kuu likiwa ni kuhakikisha mazingira ya nchi yanaendelea kulindwa na kusimamiwa ipasavyo, kwa kuzingatia miongozo ya kitaifa na kimataifa.

“Katika utekelezaji wa Miradi ya Tathmini ya Athari kwa Mazingira (TAM) Baraza limesajili jumla ya miradi 8,058, ambapo kati ya hiyo, 5,784 ni ya Tathmini ya Athari kwa Mazingira (TAM) na 2,274 ni ya Ukaguzi wa Mazingira.

“Vikao 3,836 vya wataalam vilifanyika kwa ajili ya kufanya mapitio ya taarifa za TAM na Ukaguzi wa Miradi na kutoa mapendekezo ya maboresho ya masuala ya msingi ya kuzingatiwa katika taarifa hizo.

“Miradi 4,570 iliidhinishwa na kupewa vyeti vya mazingira.

“Kati ya hivyo, 3,058 ni vya TAM, 765 ni vya Ukaguzi, huku vyeti vingine vikiwemo vya kubadili masharti 169, vyeti vilivyohamishwa umiliki 552, vyeti vya muda (PEC) 53 na cheti kilichorudishwa (certificate of surrender) 1″ameeleza Dk Semesi

Ameaema kuwa katika kuboresha utoaji wa huduma za vibali vya TAM, Baraza lilianzisha mfumo wa kielectroniki unaotumika kusajili hadi kuidhinishwa kwa miradi ya TAM ambao umeongeza ufanisi.

Ameeleza kuwa Kabla ya mfumo Baraza lilikuwa linasajili takribani miradi 900 kwa mwaka na baada ya mfumo Baraza linasajili zaidi ya miradi 2,000 kwa mwaka, jambo ambalo aliawma ni mageuzi makubwa ya Serikali ya awamu ya Sita.

“Vilevile, kaguzi zilifanyika katika maeneo 178 ya uzalishaji na usambazaji wa mifuko ya plastiki, ambapo maeneo 57 yalikutwa na makosa na kuchukuliwa hatua stahiki za kisheria.

“Zaidi ya Tani 150 za vifungashio visivyokidhi viwango vilikamatwa, vikataifishwa na kuteketezwa kwa mujibu wa Sheria”ameeleza Dk.Semesi.

About The Author

error: Content is protected !!