
BOHARI kuu ya dawa MSD imesema kuwa kipindi cha Julai mwaka jana mpaka sasa imeokoa kiasi cha shilingi Bilion 15.8 kutokana na kubana matumizi yasiyokuwa ya lazima. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea)
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Mavere Tukai akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa Bohari ya Dawa katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita leo Machi 19, 2025, katika Ofisi za Idara ya Habari – MAELEZO, jijini Dodoma.
Amesema kuwa MSD katika kuhakikisha inafanya kazi kwa misingi ya kuwa wafanisi imepunguza matumizi yasiyokuwa ya lazima na kupelekea kiasi hicho cha fedha.
Pamoja kuokoa fedha ambazo zilikuwa katika mfumo wa matumizi yasiyokuwa ya lazima pia mfumo wa matumizi ya TEHAMA umezaidia kudhibiti upoteaji wa dawa na vifaa tiba au udanganyifu ambao ulikuwa ukijitokeza.
Amesema.kuwa kwa kipindi cha miaka 4MSD imefanikisha kupeleka dawa na vifaa tiba katika vituo vyote vya afya nchini na kwa wakati jambo ambalo halijawahi kutokea kwa miaka ya nyuma.
Aidha amesema kuwa kwa sasa nchini kuna vifaa vya kisasa vya kuchuja damu na kwa kuwa na vifaa hivyo imepunguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya fedha ambazo zingetumia kwa ajili ya matibabu ya nchi.
ZINAZOFANANA
Chadema: Tundu Lissu yupo gerezani Ukonga
Serikali yajivunia mafanikio sita ya TASAF
Dk. Kimei aweka rekodi ya utendaji Vunjo