March 21, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

TAZARA sasa ipo chini ya usimamizi wa China

 

MAMLAKA ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) imetangaza kuwa Kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) itachukua usimamizi na uendeshaji wa reli hiyo kwa kipindi cha miaka 27 huku TAZARA ikifanya kazi kwa karibu kuhakikisha utekelezaji mzuri wa mradi huu. Anaripoti Apaikunda Mosha, Dar es Salaam … (endelea). 

Makubaliano hayo yamefanyika katika kongamano la kimataifa la Madini na Nishati la Zambia (ZIMEC) Alhamisi tarehe 20 Machi 2025 yakihudhuriwa na Mkurugenzi mkuu wa TAZARA na  Mtendaji Mkuu, Bruno Ching’andu.

Mamlaka hiyo imeeleza kuwa uwezkezaji huo mkubwa wenye thamani ya Dola 1.4 bilioni ni fursa ya kurekebisha miundombinu ya reli na kuboresha ufanisi wake na hivyo kuashiria sura mpya ya mfumo wa reli ya zamani.

Akizungumza na umati wa wawekezaji na wataalamu katika sekta hiyo, Ching’andu amesema sehemu ya uwekezaji utajumuisha ukarabati wa reli, pamoja na ununuzi wa vichwa vipya na mabehewa, Hatua hii inatarajiwa kuboresha usalama na kupanua uwezo wa usafirishaji wa abiria na mizigo.

Aidha, mkataba huu wa miaka 27 unalenga kutoa huduma bora zaidi na kudumisha operesheni za TAZARA, hivyo Serikali ya Tanzania na Zambia kupitia mradi huu zinatarajia ongezeka kubwa la biashara pamija na kuimarisha usafiri kati ya nchi hizi mbili.

About The Author

error: Content is protected !!