
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa serikali kwa kutambua umuhimu wa VETA imeongeza bajeti katika sekta hiyo kwa asilimia 57.4, yaani kutoka Sh. 54 bilioni mwaka 2021 hadi kufikia kiasi cha Sh. 85 bilioni kwa mwaka wa fedha 2024/2025. Anaripoti Apaikunda Mosha. Dar es Salaam … (endelea).
Akizungumza kwenye ufunguzi maadhimisho ya miaka 30 Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) yanayofanyika leo tarehe 18 Machi 2025 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu ameeleza kuwa katika zama hizi ambazo kuna kasi kubwa ya maendeleo ya kiteknolojia ni muhimu sana kwa VETA kuendelea kujiimarisha pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya kiteknolojia ili kufikia mahitaji ya soko la ajira.
Pia amesisitiza kuwa mwenendo wa kidunia unavyoonesha mafunzo ya ufundi stadi kama nguzo muhimu katika kutengeneza fursa za ajira na kukuza uchumi wa nchi yoyote ile duniani, kwa sababu yanatoa fursa kwa wahitimu wa VETA kupata ajira au kujiajiri kwa wepesi katika sekta zinazohitaji stadi za kiufundi.

Hata hivyo amewataka wadau wa elimu na mafunzo ya ufundi stadi kuhakikisha kwamba mafunzo yanayotolewa yananazingatia mahitaji halisi ya soko la ajira.
Aidha, Majaliwa ameitaka Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kutoa mafunzo yanayoendana na mabadiliko ya kiteknolojia ili wahitimu waweze kufanyia kazi ujuzi wanaoupata huku ukiwa unaendana na teknolojia za kisasa ambao utsaidia wahitimu kufanya uzalishaji wenye tija kutokana na ujuzi wanaovuna VETA.
Majaliwa amesema kupitia maadhimisho haya ni fursa ya kuitangaza veta yenyewe shughuli zake, aina ya mafunzo yanayotolewa pamoja na sifa za kwenda kusoma VETA, hivo ameitaka mamlaka hiyo kutangaza fursa za masomo zilizopo ili hata vijana wa vijijini waweze kutumia fursa hiyo kujiunga na VETA.
ZINAZOFANANA
SBL yawawezesha wanawake, vijana wa Kanda ya Ziwa kupitia ‘Training for Life’
Serikali kuwapa ulinzi wabunifu wa vifaa mbalimbali
Kauli ya Waziri Mkuu ya kusoma Veta ina siri kubwa