
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Deogratius Ndejembi amesema serikali ya awamu ya sita imefanya mageuzi ambayo yalikuwa hayafanyiki katika sekta ya ardhi hapa nchini katika kipindi cha muda mrefu. Anaripoti Apaikunda Mosha, Dodoma … (endelea).
Amezungumza hayo 17 Machi 2025 wakati wa uzinduzi wa sera ya ardhi ya mwaka 1995 toleo la mwaka 2023, kwenye kituo cha mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma.
Ndejembi amesema pindi Rais Samia ameingia madarakani alitoa mapendekezo kwa wizara hiyo ya kupanga, kupima na kumilikisha ardhi kwa watu, na kufikia hivi sasa yamefanyika kikamilifu.
Aidha, ameeleza kuwa takribani bilioni 50 zimetolewa na serikali katika mfuko wa KKK, kwa ajili ya wizara ya ardhi, hivo wizara hiyo kwa kushirikiana na TAMISEMI ilifanikiwa kuzikopesha Halmashauri zaidi ya 52 kwaajili ya kupanga, kupimaji na kuzimilikisha ardhi kwenye halmashauri hizo.
Pia serikali ya awamu ya sita iliridhia kutoa Bilioni 133 kwaajili ya vitendea kazi mbalimbali vya kuboresha sekta ya ardhi nchini, ambapo kati yake fedha hizo zimewezesha kununua magari 70 ambayo yanatumika katika halmashauri ili kuwezesha utekelezaji mzuri wa majukumu ya watumishi hao.
Vilevile Ndejembi amesema Serikali ya awamu ya sita imetoa Dola za Marekani milioni 65 ambazo zimetumika kutengeneza ramani ya msingi mpya katika nchi yetu, suala ambalo kwa mara ya mwisho lilifanyika mwaka 1978.
Aidha Ndejembi, ameeleza kuwa kuna ulazima wa kuhakikisha ardhi ya nchi inapimwa licha ya kuwa na ardhi na mipaka ile ile kutokana na ongezeko la watu kila wakati jambo ambalo litasaidia kutambua kwa haraka kila maeneo ili yatunzwe na yarithishwe kwa vizazi vitakavyokuja.
ZINAZOFANANA
Bil 3.4 zatumika kulipa fidia wamiliki wa ardhi Dodoma
NSSF kutoa mafao siku moja baada ya mwanachama kustaafu
Serikali kuwapa ulinzi wabunifu wa vifaa mbalimbali