March 18, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Kauli ya Waziri Mkuu ya kusoma Veta ina siri kubwa

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Anthony Kasore

 

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Anthony Kasore, amesema VETA inawapa watu uwezo wa kufanya shughuli mbalimbali kwa vitendo hivo wanaotakiwa kupata ujuzi huu ni watu wa Elimu zote.  Anaripoti Apaikunda Mosha, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza mapema leo 17 Machi 2025 katika moja ya vyombo vya habari Kasore ameisistiza kuwa kauli ya Waziri Mkuu Majaliwa imebeba moja ya siri kubwa sana ambayo haikuwahi kutolewa hata na VETA, hivo wale wanaojitambua wataona umuhimu wa kutafuta ujuzi huo.

“Sera mpya ya elimu inahimiza elimu ya ujuzi, ndio maana sasa tunazungumzia elimu ya amali na mabadiliko haya yatasaidia kuzalisha watu wenye ujuzi na uwezo wa kushiriki kikamilifu katika shughuli za uchumi,” amesema Kasore.

Kuelekea katika kilele cha maadhimisho ya miaka 30 ya VETA Kasore amesema yapo mabadiliko mengi ambayo taasisi hiyo imefanya ili kufikia mahitaji ya soko la ajira, amesema maboresho katika mitaala inayotelewa inahakikisha mafunzo ya VETA yanaendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia ili kuendana na mahitaji ya soko la ajira.

Aidha Kasore anawaalika wananchi wote katika maadhimisho hayo  ambayo yataangazia katika mifumo ya ufundishaji, kuangazia wanufaika wa VETA na katika mifumo ya ajira na waajiri kuponyesha watu wanaowahitaji pamoja na midahalo yote ni kuhakikisha eneo la ufundi stadi linatengeneza watu mahiri na ajira za kutosha.

About The Author

error: Content is protected !!