March 18, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Hakuna sheria inayomkataza mwanamke kumiliki ardhi

 

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema hakuna sheria inayomkataza mwanamke kumiliki ardhi kwani naye ana haki ya kupata ardhi kama ilivyo kwa mtu yoyote yule kwa kuzingatia taratibu za nchi. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Rais Samia ametoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa Sera ya Taifa ardhi ya mwaka 1995 toleo la mwaka 2023 katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.

Amesema kuwa mwanamke naye ana haki ya kumiliki ardhi kwa kufuata misingi na taratibu na sheria za nchi kama alivyo mtu mwingine yoyote ilimradi awe ni mtanzania.

Katika hatua nyingine amewataka watendaji katika Wizara husika kuhakikisha wanapima ardhi na kuwamilikisha wananchi kwa kulipia gharama kwa mujibu wa sheria ya nchi.

Amesema kuwa wapo watu ambao siyo waaminifu ambao wanashirikiana na watu wa ardhi kwa kufuta hati za watu na kuwapora ardhi zao na kuwapa watu wengine jambo ambalo halopendezi wala halikubaliki.

Aidha amesema ardhi itaendelea kuwa mali ya Umma huku msimamizi mkubwa akiwa Rais na ardhi itakodishwa wenyeji na kuhakikisha mipaka inatambuliwa vyema .

About The Author

error: Content is protected !!