March 14, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Watanzania watakiwa kuipiga chini CCM

 

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Taifa (Bara), Omar Dunga amepokelewa katika wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma huku akiwataka Watanzania kufanya mabadiliko ya kuwachagua wabunge na madiwani wanaotokana na chama hicho ili wakazuie bajeti zinazowakandamiza Watanzania. Anaripoti Danson Kaijage, Kondoa, Dodoma … (endelea).

Akizungumza na wananchi katika uwanja wa stendi ya zamani Dunga amewataka wananchi kuchagua wabunge na madiwani ili wakazuie bajeti zinaxowakabili wananchi. Alisema kuwa chama hicho kitashiriki uchaguzi Mkuu wa Rais Wabunge na Madiwani.

Amesema kuwa kwa sasa asilimia 99 ya wabunge wanatatokana na Chama cha Mapinduzi (CCM), kuwa iwapo wananchi watakichagua chama hicho, watauza mazao yao vizuri,tofauti na sasa wananchi wanalazimishwa kuuza mazso kwa kutumia mfumo wa stakabadhi ghalani ambapo wamekuwa wakiuza kwa mkopo.

“Hospitali nyingi zimejengwa lakini hakuna huduma,hakuna dawa lakini CUF itahakikisha huduma zinaboreshwa hasa vijijini ambapo wananchi wamekuwa wakipata adha kufika kwenye vituo vya kutolea huduma kutokana na ubovu wa miundombinu ya barabara, “ameeleza.

Amewaeleza wananchi kwa kuwaambia kuwa umaskini wa wananchi sio laana ya Mungu, CUF ikishika dola itafanikisha mambo mengi ikiwemo wazee watapata posho ya kujikimu kila mwezi, “alisema.

Dunga amesema kuwa elimu bure haijaleta matokeo mazuri kwa wananchi kutokana na shule nyingi kuwa na michango mingi inayozidi hata ada zilizoondolewa.

Katika mkutano huo zaidi ya wanachama wapya 20 walikabidhiwa kadi. Mkazi wa Kondoa, Hamidu Mkopi alitaka wananchi kuziishi 4R za Rais Samia Suluhu Hassan.

About The Author

error: Content is protected !!