March 13, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

TBA warejea kazini kukamilisha nyumba 3,500 Dodoma

 

WAKALA wa Majengo Tanzania (TBA) wameanza kutekeleza awamu ya pili ya mradi wa ujenzi wa nyumba 3,500 za Makazi ya Watumishi wa Umma eneo la Nzuguni ‘B’ jijiini Dodoma. Anaripoti Apaikunda Mosha, Dodoma … (endelea).

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) wakati wa ziara yake leo 13 Machi 2025  ya ukaguzi wa nyumba hizo imeipongeza (TBP) kwa utekelezaji wa mradi wa ujenzi kwa Awamu ya Pili wenye nyumba 60 za chini na maghorofa matatu ambazo zikikamilika kwa awamu zote zitakuwa jumla ya nyumba 3,500.

Akizungumza ma vyombo vya habarii mara baada ya kukagua mradi huo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Augustine Vumma amesema kuwa mradi wa awamu ya kwanza wenye jumla ya nyumba 150 umekamilika na  asilimia 90 ya nyumba hizo zina wapangaji zote.

Aidha, Vumma ameipongeza serikali kupitia wizara ya ujenzi wakishirikiana na TBA kwa ubunifu mzuri wa mradi mkubwa na wa kimkakati ukizingatia Dodoma ni jiji ambalo kwa sasa limefurika idadi kubwa ya watu kwahiyo kumekuwa na uhitaji mkubwa wa nyumba hivyo upangiliaji wa kimkakati wa nyumba hizo umefanya zilete tija.

Kwa upande wake, Kaimu Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Idara ya Ufundi na Umeme wa Wizara ya Ujenzi, Mwanahamisi Kitogo amesema kufuatilia maelekezo hayo yaliyotolewa ni nyongeza ya sera zilizokuwepo hivo  watachukua jukumu la  kuzisimamia na kutekeleza maelekezo hayo.

Naye, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Daud Kondoro amesema kuwa utekelezaji wa mradi huo pia utahusisha ubia kati ya Wakala huyo na Sekta Binafsi lengo ni kuhakikisha kuwa mradi huo unatekelezwa kwa haraka na ufanisi.

About The Author

error: Content is protected !!