March 13, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Taasisi za dini zinazofanya biashara zatakiwa kulipa kodi

Kamishina wa TRA, Yusuph Mwenda

 

TAASISI za kidini zinazofanya biashara badala ya kutoa huduma zinatakiwa kulipa kodi ya Serikali na si vinginevyo. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea)

Hayo yamebainishwa jana na Kamishina wa TRA, Yusuph Mwenda wakati alipokuwa anatoa taarifa ya maendeeo kwa waandishi wa habari katika ukumbi wa Habari Maelezo Jijini Dodoma juu ya mafanikio ya Mamaka hiyo kwa kiindi cha miaka 4 ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Kamishina huyo alilazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya kuulizwa swali na mwandishi wa habari wa chombo hiki aliyetaka kujua ni utaratibu gani kwa taasisi za dini ninazojenga vitaga uchumi na kuwakodosha wafanya biashara.

Kamishina huyo amesema kuwa taratibu zinaonesha wazi kwamba taasisi za Dini zinazotoa huduma zinapewa misamaha ya kodi.

“Tunatoa misamaha ya kodi kwa taasisi zinazotoa huduma lakini kama taasisi inafanya biasha au imejenga jengo na inakodisha inatakiwa kulipa kodi kwani taasisi hiyo inafanya boashara.

Katika hatua nyingine ameendelea kuwasisitiza watanzania kuhakikisha wanalipa kodi kwa hiari kwa faida ya maslahi mapana kwa taifa.

About The Author

error: Content is protected !!