March 13, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Mbogamboga, vitunguu yaingiza Mil 370

 

MAZAO ya Mbogamboga pamoja na vitunguu vinavyozalishwa nchini Tanzania ni sehemu ya maendeleo na kuchangia pato la taifa kwa kipindi cha miaka 4 ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TANTRADE), Latifa Mohamed Khamis, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa mamlaka hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita katika Ofisi za Idara ya Habari – MAELEZO, jijini Dodoma.

Akielezea mafanikio katika kipindi hicho amesema Maonesho ya Mbogamboga Expo Doha, 2023/24 Kampuni 13 zilishiriki na kufanikisha mauzo ya papo kwa papo ya Sh. 370 milioni.

Ameeleza kuwa fursa za mauzo za Sh.  125 milioni zilifunguliwa kupitia mazungumzo ya kibiashara.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TANTRADE), Latifa Mohamed Khamis

Akiendelea kuelezea mafanikio kwa Mamlaka hiyo amesema kwamba Kampuni za Qatar zilionesha nia ya kuwekeza katika usindikaji wa chakula na usimamizi wa taka.

Aidha amesema maonesho ya Biashara ya Afrika (AfCFTA Exhibitions on Intra-Africa Trade) ya mwaka 2023 ambapo,
Mauzo ya papo kwa papo yenye thamani ya Shilingi bilioni 2.17 yalifanyika na kuongeza kuwa Mikataba ya biashara yenye thamani ya Sh. 17 bilioni ilisainiwa.

“Katika kipindi hiki, TanTrade imefanikiwa kupanua masoko, kusaidia biashara za Tanzania kupata fursa za kimataifa, kujenga uwezo wa wafanyabiashara wadogo na wa kati, na kuboresha mifumo ya upatikanaji wa taarifa.

Ameeleza kuwa uratibu wa DITF ambao ulipelekea mafanikio kwa kipindi cha mwaka 2020/21 -2023/24,washiriki wa ndani wameongezeka kutoka 2,926 hadi 3,503, huku washiriki wa nje wameongezeka kutoka 76 hadi 451.

About The Author

error: Content is protected !!