March 12, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Watanzania wawili wamegundulika kuwa na virusi vya Mpox

 

WAZIRI wa Afya, Jenista Mhagama, amethibitisha kuwa wahisiwa wawili wana maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Mpox baada ya sampuli zao kuchukuliwa na kupelekwa maabara ya Taifa kwa chunguzi, mnamo tarehe 9 Machi, 2025. Anaripoti Apaikunda Mosha. Dodoma … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na wizara ya afya tarehe 10 Machi 2025 inaeleza kuwa wizara ya afya kupitia mifumo yake ya ukusanyaji taarifa na ufuatiliaji wa magonjwa ilipokea taarifa za uwepo wa wahisiwa wenye dalili za vipele usoni, mikononi, miguuni na sehemu nyingine za mwili. Dalili hizi ziliambatana na homa, maumivu ya kichwa, vidonda kooni, maumivu ya viungo vya mwili ikiwemo misuli na mgongo.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa chanzo cha ugonjwa huu ni wanyama jamii ya nyani, ambapo binadamu huweza kuupata kutokana na shughuli zinazoweza kusababisha kugusana na wanyama, majimaji au nyama za wanyama wenye maambukizi. Aidha, endapo binadamu akipata maambukizi hayo anaweza kumwambukiza mtu mwingine kwa kugusana moja kwa moja.

Aidha, Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI na vito vyote vya kutolea huduma za Afya, inaendelea na fuatiliaji, uchunguzi na utambuzi kubaini kama kuna wahisiwa wengine ili waweze kupatiwa huduma stahiki.

“Kwa taarifa hii, Wizara ya Afya, inawahakikishia wananchi kuwa Serikali imejipanga kudhibiti ugonjwa huu na hasa kutokana na uzoefu tulionao wa kudhibiti magonjwa ya mlipuko. Serikali inaendelea kuimarisha ufuatiliaji wa magonjwa katika ngazi zote, upimaji wa watu wanaoingia na kutoka kupitia mipaka ya nchi, kumarisha utoaji wa elimu ya afya na kuhamasisha jamii ili kuwawezesha wananchi kuchuka hatua za kujikinga.”

Vilevile taarifa inaeleza kuwa kwa kuzingatia uwepo wa magonjwa mengi yanayosababishwa na virusi kutokuwa na tiba mahususi, mgonjwa anahudumia kulingana na dalili alizonazo, hivyo Wizara inawasihi na kuwasisitiza wananchi wote kuzingatia na kutekeleza hatua za kujikinga.

About The Author

error: Content is protected !!