March 10, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Asilimia 22 ya vijana wanakumbwa na magonjwa yasiyo ya kuambukizwa

Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Dk. Irene Isaka

 

ASILIMIA 22 ya vijana wanakabiliwa na magonjwa yasiyokuwa ya kuambukizwa hivyo ni muhimu kukata bima ya afya kwa ajili ya usalama wao pindi watakapokumbwa na magonjwa hayo. Anaripoti Danson Kaijage Dodoma … (endelea).

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Dk. Irene Isaka wakati wa mkutano na waandishi wa habari kwa lengo la luelezea utekelezaji wa maendeleo kwa kipindi cha miaka 4 inayoongozwa na Rais aliyepo madaeakani uliofanyika katika ukumbi wa Mkutano wa Habari Maelezo Jijini Dodoma.

Dk. Irene amesema kuwa utafiti uliofanywa kwa kipindi cha mwaka 2021/22 umeonyesha kuwa asilimia 22 ya vijana wanatatizo la magonjwa yasiyokuwa ya kuambukizwa.

Amesema kuwa pamoja na kusumbuliwa na magonjwa yasiyokuwa ya kuambukizwa pia kuna tatizo kubwa kwa vijana ambalo ni tatizo la afya ya akili.

Kutokana na hali hiyo watanzania wote wametakiwa kukata bima ya afya ya NHIF wakati wakiwa na afya badala ya kusubiri waanze kupata tatizo la kiafya jambo ambalo haliwezi kuwasaidia kwa ufasaha kama ambavyo wangekata bima wakati wakiwa na afya njema.

Akizungumzia zaidi juu ya mafanikio kwa kipindi cha miaka hiyo mnne Dk. Irene amesema kuwa mfuko huo umefanikiwa kuimarisha mifumo ya TEHAMA katika shughuli za mfuko ili kuimarisha utendaji na tija.

Amesema uhimarishaji wa TEHAMA umesaidia mwananchi kuweza kujisajili ili kujiunga na mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya kwa kutumia mfumo wa mfumo huo.

Aidha ameeleza kuwa kwa sasa malipo ya watoa huduma yanafanyika kwa wakati kwa sababu ya uwepo wa mifumo ya TEHAMA.

Amesema kuwa madai ya watoa huduma za afya yanafanyika ndani ya siku 60 ikilinganishwa na siku 120 za awali kabla ya uwepo wa mifumo

Akiendelea kufafanua mafanikio hayo amesema kuwa katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita wamesajili wanachama milioni 2.2

Akizungumzia ukusanyaji wa michango amesema, ukusanyaji wa michango umefikia trilioni 2.3 kwa sasa kutokana na maboresho yaliyofanyika katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita.

Amesema kuwa ulipaji malipo ya watoa huduma unafanyika kwa wakati kwa kuzingatia huduma mpya za afya zinazotolewa.

Aidha amesema kuwa Sh. 2.29 trilioni zimelipwa kwa watoa huduma waliohudumia wanachama wa NHIF.

Pia ameelezea kuwa Sh. 91 bilioni zimelipwa kwa watoa huduma waliohudumia wanachama wa NHIF ambao ni wastaafu.

Akiendelea kutoa ufafanuzi wa mafanikio hayo amesema kuwa Sh. 22 bilioni zimeokolewa kutokana na usimamizi madhubuti wa mfuko wa NHIF, fedha hii ilikuwa inapotea kutokana na udanganyifu wa baadhi ya wanachama

Hata hivyo amesema kuwa watumishi 36 wa vituo vya kutolea huduma wamechukuliwa hatua kwa kufanya udanganyifu kwenye mfuko.

Katika mafanikio hayo amesema kuwa Mfuko una ziada ya bilioni 95 kwa sasa ikilinganishwa na kipindi cha nyuma ambapo ulikuwa na nakisi.

About The Author

error: Content is protected !!