
JUMUIYA ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) inatarajia kufanya mkutano mkuu wa 39 wa kikatiba wa mwaka, jijini Dodoma, tarehe 11 Machi siku ya Jumanne kwa lengo la kupitia agenda mbalimbali za kimaendeleo pamoja na kujadili ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti wa hesabu za Serikali (CAG). Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa ALAT, Murshid Ngeze alipokuwa akizungumza na nyombo vya habari kuhusu maadalizi ya Mkutano huo ambao unatarajiwa kufanyika Jijini Dodoma huku Mgeni rasm akitarajiwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan.
Amesema mkutano huo utakuwa na mambo mengi ya kujadili ikiwa ni pamoja na kuhuisha Jumuhiya hiyo sambamba na kupitia utekelezaji wa kutaka kuanzisha ujenzi wa kitega uchumi kwe kiwanja chao chenye ukubwa wa mita za Mraba 6000.
“Katika mkutano huo pia tutajadili na kutathinini,kukichunguza katika utendaji wetu katika halmashauri.
“Kutoa taarifa za mapato na matumizi,kujua kila kata inapata kiasi gani cha fedha za maendeleo pamoja na kujua na kutoa majibu ambayo yalikuwa na dukuduku,” ameeleza Ngeze.
Aidha amesema kuwa mkutano huo utakuwa nanjukumu la kujadili na kupitisha bajeti sambamba na kueleza mapato na matumizi kwa lengo la kuweka uwazi kwa jamii.
Ngeze amesema kuwa mkutano huo ambao ulikuwa ufanyike Jijini mwanza umebadilishwa na utafanyika Jijini Dodoma baada ya kupewa ushauri na TAMISEMI kutokana na ratiba nyingi za atakaye kuwa mgeni rasm ambaye ni Rais Samia.
Akizungumzia maadalizi Ngezi amesema kuwa mpaka sasa ALAT imefanikiwa kuharika wageni mbalimbali kutoka nje ya nchi na ndani ya nchi.
ZINAZOFANANA
Papa Francis amteua Askofu Musomba kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo jipya la Bagamoyo
NBC yaandaa hafla ya futari Zanzibar, yajivunia ongezeko la wateja
BUWASSA yapewa Bil 28.1 kutatua tatizo la maji Bunda