
PAPA Francis
PAPA Francis amewashukuru waumini na wasio waumini wa Kanisa Katoliki kwa kuendelea kumuombea afya njema tangu alipolazwa Februari 14,2025. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa, Rome Italia … (endelea).
Papa Francis (88) amelazwa katika Hospitali ya Gemelli mjini Roma akisumbuliwa na maradhi kwenye mfumo wa upumuaji. maradhi hayo yamesababisha asionekane hadharani kwa zaidi ya wiki tatu.
Katika ujumbe wake wa sauti (audio) kwa waumini alioutoa jana jioni Machi 6,2025, Papa Francis, amesikika akizungumza japo kwa shida. Kauli yake hiyo imeelezwa kuwarejeshea matumaini waumini wa kanisa hilo ambao wamekuwa wakitumia muda mwingi kumuombea apone.
Hotuba ya Papa Francis, iliyorekodiwa na kutangazwa kupitia vipaza sauti katika uwanja wa Mtakatifu Petro huko Vatican kabla ya sala ya Rozari ya jana jioni, ilikuwa mara ya kwanza kwa wafuasi wake kusikia sauti yake tangu alazwe hospitalini takriban wiki tatu zilizopita.
“Nawashukuru kwa dhati kwa maombi yenu kwa ajili ya afya yangu kutoka uwanjani nami nawasikiliza kutokea hapa hospitalini. Mungu awabariki na Bikira Maria awalinde. Asanteni,” alisema Papa Francis, akizungumza taratibu kwa lugha ya Kihispania ambayo ni lugha yake ya asili.
ZINAZOFANANA
Kamati ya Ligi yaufuta mchezo wa Yanga na Simba
Bodi ya Ligi: Mchezo upo palepale, Yanga hawachezi siku nyingine
Simba yasusia mchezo wa Derby, sababu hii hapa