March 9, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

NBC yaandaa hafla ya futari Zanzibar, yajivunia ongezeko la wateja

 

BANKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imeandaa hafla ya futari mahususi kwa wateja wake wa Kiislamu Zanzibar huku ikijivunia ongezeko la wateja visiwani humo kutoka wateja 22,196 mwaka jana hadi zaidi ya 34,942 mwaka huu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Hafla hiyo imefanyika jana Hotel Verde, Zanzibar ikiongozwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi -Zanzibar, Zubeir Ali Maulid, Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya NBC, Rayson Foya alimuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Theobald Sabi kwenye hafla hiyo iliyohudhiriwa na wateja, viongozi wa serikali pamoja wafanyakazi wa benki ya NBC.

Katiba hotuba yake Spika Zubeir aliipongeza benki hiyo kwa muendelezo wake wa kutumia mwezi Mtukufu wa Ramadhani kujenga mahusiano yake na wateja wenye imani ya Kiislam, hatua aliyoitaja kuwa imekuwa ngunzo muhimu katika ustawi wa biashara sambamba na kuchochea uchumi jumuishi kupitia huduma bora za kibenki.

Spika wa Baraza la Wawakilishi, Zubeir Ali Maulid akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na NBC

“Ni wazi kwamba benki ya NBC wanatambua kuwa Ramadhan ni nguzo muhimu ya imani ya Kiislamu, wakati wa ibada, upendo, na sadaka. Hivyo kwa kutambua thamani hiyo, futari hii ni ishara ya kuthamini mahusiano yao na sisi wateja wao na wadau wao, ikiwa ni njia mojawapo ya kushirikiana pamoja baraka za mwezi huu,’’ alisema Spika Zubeir.

Akizungumzia mafanikio na ongezeko la wateja hao, Foya alisema limechochewa zaidi na mahusiano mazuri baina ya benki hiyo na wateja visiwani Zanzibar hususani kupitia utoaji wa huduma unaozingatia misingi ya Sharia za La’ Riba sambambamba na maboresho ya huduma za benki hiyo hususuani kwa njia kidigitali.

Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya NBC, Rayson Foya akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na NBC

“Katika kuthibitisha dhamira yetu kwenye maboresho ya huduma zetu ni hivi karibuni tu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alizindua rasmi ‘App yetu ya NBC Kiganjani ikiwa na maboresho makubwa zaidi kulingana na mahitaji ya wateja wetu ambao sasa wanaweza kufungua akaunti popote walipo, kufanya malipo ya serikali (GEPG), kununua umeme (LUKU), na kulipa ankara mbalimbali kwa urahisi. Nawaalika wote kupakua NBC Kiganjani App kutoka Google Play Store au Apple App Store na kufurahia huduma hii ya kisasa,’’ alisema.

Hafla hiyo pia ilihusisha utoaji wa zawadi kwa wageni waalikwa huku pia ikitoa wasaa kwao kubadilishana mawazo na kufurahia pamoja wakati huu wa mfungo wa Ramadhani.

Spika wa Baraza la Wawakilishi -Zanzibar, Zubeir Ali Maulid (katikati) akipokea zawadi maalum kutoka kwa Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya NBC, Rayson Foya (kushoto)

About The Author

error: Content is protected !!