
Mkurugenzi wa BUWASSA, Esther Gilyoma
MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mji wa Bunda (BUWSSA),kwa muda wa miaka 4 ya uongozi wa Raisi, imepitishiwa miradi ya thamani ya Sh. Bilioni 28.1 na Sh.Bilioni 11.89 taryari zimepokelewa na baadhi ya miradi imekamilika na mingine utekelezaji unaendelea. Anaripoti Danson Kaijage,Dodoma … (endelea).
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma Mkurugenzi wa BUWASSA, Esther Gilyoma kwa lengo la kutoa taarifa ya mafanikio ya kwa kipindi cha miaka 4 ya uongozi wa Rais Samia katika ukumbi wa habari Maelezo amesema Mamlaka hiyo imeweza kuwafikia wanancho wengi kihuduma.
Esther amesema kuwa ndani ya miaka minne ya Mamlaka hiyo imepokea kiasi cha Sh. 11.89 bilioni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji na baadhi imekamilika na mingine inaendelea kutekelezwa ili wananchi wapate huduma ya majisafi na salama.
Ameeleza kuwa alisema Mamlaka hiyo imepitishiwa miradi ya thamani ya Sh. 28.1 bilioni na Sh. 11.89 bilioni na taryari fedha hizo zimepokelewa na baadhi ya miradi imekamilika na mingine utekelezaji unaendelea.
Ameeleza kuwa miongoni mwa miradi iliyokamilika ni Mradi wa ujenzi wa chujio la maji Nyabehu – Bunda ambayo umegharimu Sh. 10.6 bilioni na wananchi 227,446 wananufaika na mradi huo.
Amesema Mradi wa Miundombinu ya Majitaka Butakale – Bunda utekelezaji wake umefikia asilimia 46 na unagharimu Sh.Bilioni 1.72 huku wananchi 227,446 wanatarajiwa kunufaika.
Alitaja mradi mwingine ni ujenzi wa Maji Balili, Rubana na Kunzugu – Bunda umekamilika na umegharimu Sh. 759.8 milioni na wananchi 7,699 wamenufaika, Mradi wa Ujenzi wa Maji Manyamanyama Mugaja – Bunda, umekamilika ambao umegharimu Sh. 1.13 bilioni na wananchi 7,012 wamenufaika.
Amesema kuwa Mradi wa ujenzi wa maji Misisi- Zanzibar Mjini Bunda umegharimu Sh. 733.24 milioni na wananchi 7,042 wamenufaika na huduma ya majisafi na salama huku Mradi wa Kusambaza maji Wariku utekelezaji wake umefikia asilimia 40 na wananchi 33,088 wanatarajiwa kunufaika.
Pamoja na miradi hiyo, alisema kuna Mradi wa kusambaza maji Kisangwa umegharimu Sh. 716 milioni na wananchi 20,688 wanatarajiwa kunufaika ambapo utekelezaji umeanza na upo asilimia sita, Mradi wa kusambaza maji Migungani Kaswaka unagharimu Sh. 1.2 bilioni na watanufaika wananchi 37,058, Mradi wa kusambaza maji Nyamswa Bunda utagharimu Sh. 8.3 bilioni na watanufaika wananchi 51,935.
Mkurugenzi huyo amesema.Mamlaka ina mipango mbalimbali kwa ajili ya kuhakisha huduma inazidi kuinaimarika mjini Bunda kwa mwaka wa fedha 2025/26 ikiwamo ujenzi wa mfumo wa wa mtandao wa maji taka, ujenzi wa tangi kubwa la maji kwenye mwinuko lenye uwezo wa kubeba lita milioni tano, ujenzi wa tangi kubwa la maji lenye uwezo wa kubeba lita 670,000 kwenye kituo cha kusukuma maji Migungani.
Mkurugenzi hyo amesema kuwa wanapanga kujenga tangi kubwa lenye uwezo wa kubeba lita 225,000 kwenye kituo cha kusukuma maji Mugaja, kujenga tangi la maji lenye uwezo wa kubeba lita 150 Kisangwa, kujenga upanuzi mtandao wa bomba 300mm kutoka Migungani hadi Mlima bomani na kujenga mtandao wa bomba toka kituo cha kusukuma maji Migungani hadi mlima Nyendo.
ZINAZOFANANA
Serengeti yatambuliwa Tuzo za Rising Woman kwa kukuza usawa wa kijinsia
ALAT kujadili ripoti ya CAG
Papa Francis amteua Askofu Musomba kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo jipya la Bagamoyo