
TAASISI ya Tiba ya Mifupa, ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu (MOI) kwa miaka minne ya uongozi wa Ras Samia Suluhu Hasani imefanikiwa kuokoa kiasi cha Sh. 150 bilioni kwa ajili ya wangonjwa ambao wangetibiwa nje ya nchi. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).
Hayo yamebainishwa na Balozi, Dk. Mpoki Ulisubisya, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya MOI alipokuwa akitoa taarifa kwa vyombo vya habari katika ukumbi wa Habari Maelezo Jijini Dodoma, juu ya mafanikio ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Akitoa taarifa ya mafanikio Dk. Ulisubisya amesema kuwa kwa kipindi cha miaka minne Taasisi hiyo imeweza kutoa huduma bingwa za kimatibabu na kuweza kuokoa mabilioni ya fedha kwa wagonjwa ambao wametibiwa ndani ya nchi badala ya kutibiwa nje ya nchi.
Katika huduma muhimu zinazotolewa na MOI ni pamoja na kutoa huduma ya mkono wa umeme ambapo mpaka sasa wagonjwa sita wamewekewa mkono bandia.
Amesema kuwa kutengeneza viungo bandia kwa teknolojia ya ‘3D’ kwa wagonjwa wanne (4).
Pia amesema kuwa MOI imeanzisha huduma mpya za kibingwa na kibobezi ambazo hazipatikani hapa nchini kama vile Bone Bank na matibabu ya Parkinsons disease na kutetemeka ndani ya miaka mitatu.
Amesema kuwa Katika kipindi hiki cha miaka minne MOI imefanikisha kuanzisha na kuendeleza mambo mbalimbali kama vile, kuanzisha huduma mpya za kibobezi,upanuzi wa miundombinu Upatikanaji wa vifaa tiba mafunzo na kupandishwa madaraja watumishi.
Amesema kuwa katika kipindi cha miaka minne, Taasisi ya MOI imefanikiwa kutoa huduma za kibobezi kwa wagonjwa 7,366.
Amesema kuwa gharama za matibabu hayo ndani ya nchi zilikuwa shilingi za Kitanzania 68,451,603,600.00 na kama wagonjwa hao wangepelekwa nje ya nchi kwa matibabu jumla ya shilingi 218,280,169,470 zingetumika.
Kutokana na hali hiyo amesema kuwa serikali imefanikiwa kuokoa shilingi bilioni 149,828,565,870.00 ambazo zimetumika katika shughuli nyingine za maendeleo.
Akizungumzia mipango ya baadaye amesema Taasisi inaendelea kuboresha huduma kwa viwango vya kimataifa kwa
Ujenzi wa hospitali ya kisasa ya utengamao (Rehabilitation centre) katika kiwanja cha MOI chenye ukubwa wa hekari 10 kilichopo Mbweni Mpiji jijini Dar es salaam.
Kusogeza huduma katika jengo ambalo lilikua linatumika na Hospitali ya Tumaini upanga ili sehemu ya wagonjwa wa nje waanze kupata huduma katika jengo hilo na kupunguza msongamano MOI.
ZINAZOFANANA
Hospitali ya Benjamin Mkapa yapandikiza mimba 21, watano kuongezewa nguvu za kiume
Makusanyo ya mapato katika hospitali Magu yazidi kupaa
JKCI kinara utoaji huduma ya afya Afrka Mashariki na Kati