
WAZIRI wa Uchukuzi Zanzibar, Khalid Salum Mohammed amesema serikali haiwezi kuvunja mkataba na Mwekezaji kutoka Kampuni ya Kifaransa ya Uwendeshaji Bandarini (AGL) iliyopewa dhamana na Serikali ya Zanzibar kuendesha Bandari hiyo. Anaripoti Apaikunda Mosha, Zanzibar … (endelea).
Akizungumza na vyombo vya habari tarehe 3 Machi 2025, Khalid amesema kufuatia madai ya Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Act Wazalendo Ismail Jussa, kuitaka serikali hiyo kuvunja mkataba na mwekezaji huyo, kwa sababu ya kutoridhishwa na kutonufaika na uwekezaji huo.
Ameeleza kuwa madai ya matumizi ya kiasi cha Sh. 17 bilioni za kununulia vifaa vya bandari ilikuwa kwa ajili ya kuendesha bandari na kuboresha bandari na wakati wa ununuzi wa vifaa hivyo ulipofanyika ilikuwa kabla ya wazo la kutafuta mwekezaji kufanyika.
“Mkataba huo na masharti yake yapo, hatuwezi kusema tunavunja mkataba kwa sababu mtu mmoja au kikundi Fulani hawajaridhika, hii sio sahihi na ni upotoshaji kusema kwamba vifaa vilivonunuliwa ulikuwa ni mpango wa makusudi wa kumtengenezea mwekezaji huyu njia aje kuchukua fedha za bure,” amesema Khalid.
Amesema faida zilizopatikana katika uwekezaji huo zipo wazi na mpaka sasa mafanikio makubwa wanapata kutoka katika bandari hiyo kulinganisha na awali, ufanisi katika Bandari umeongezeka kwani hata Meli za Mizigo zinakaa siku chache Nangani tofauti na ilivyokua awali.
ZINAZOFANANA
Sekta ya madini yaoaisha pato la Taifa
Jamii yaaswa kufichua wafanyabishara za magendo Bagamoyo
Makusanyo ya mapato katika hospitali Magu yazidi kupaa