
MAMLAKA ya Mapato nchi TRA imepewa rai ya kuzungumza na wenyeji wa Bagamoyo ili kuwaelimisha juu ya athari za ukwepaji kodi na magendo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Pwani … (endelea0.
Rai hiyo imetolewa jana tarehe 3 Machi 2025 na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Shaibu Ndemanga wakati Maofisa wa Mamlaka hiyo walipokuwa wakitoa elimu ya mlipa kodi kwa wakazi wa Bagamoyo.
DC Ndemanga amesema kuwa mapato ya serikali yanayopotea kutokana na watu kukwepa kodi kwa kupitisha mizigo kwa njia ya magendo kwenye bandari ya Bagamoyo.
“Kama watu wengi kuwa wanapita pale bandarini Bagamoyo tungekuwa tunakusanya Bilioni 3 hadi 4 kwa mwezi. Unaona jahazi limetia nanga pahala ambapo sio bandari badala ya kutoa taarifa nao wanakwenda kusaidia kushusha bidhaa ili wapate chochote hawa wananchi nao wanaihujumu serikali,” amesema DC Ndemanga.
DC Ndemanga amesema kuwa Mamlaka itaendelea kutoa elimu kwa wafanyabiashara juu ya hatari ya kupitisha mizigo yao kwa njia za magendo .
“Hawa wafanyabiashara wakielewa hawatakubali mizigo yao ipitishwe njia za magendo kwa sababu tukikamata hasara itamkumba yeye na sio wale wanaowatuma,” alisema.
“Wengine wanatumia namba ya mlipa kodi ya mtu mwengine sisi tunahesabu mtu huyo naye anafanya magendo tu”, alisema DC Ndemanga
Naye Deogratius Nyenshile Ofisa wa Forodha wa TRA ambaye ndiye aliyeendesha mafunzo hayo amesema kuwa upo umuhimu kwa jamii kujua athari za kiuchumi endapo watu wanakwenda kodi.
“Mwananchi ndio mlinzi wa kwanza wasipoelimishwa wanaweza kushiriki kwenye biashara ya magendo bila yeye mwenyewe kujua kwa hiyo ni muhimu kila wakati kuwaelemisha wanachi madhala ya ukwapaji kodi na magendo kwenye ustawi wa taifa nchini,” alisema Nyenshile.
Amesema kuwa mamlaka itaendelea na jitahada hizo za kutoa elimu ili kuhakikisha wananchi wanakuwa mstari wa mbele kwenye kufichua magendo.
Naye Mwenyekiti wa Wabeba mizigo katika bandari ya Bagamoyo, Jumanne Buna ametoa malalamiko yake kuwa wafanyabiashara wadogo wanashindwa kuendelea na bishara zao kwa kutozwa kodi sawa na wafanyabiashara wakubwa.
ZINAZOFANANA
Maokoto ya uhakika na Fishtastic kasino ya uvuvi baharini
Sekta ya madini yaoaisha pato la Taifa
Serikali ya Zanzibar yagoma kuvunja mkataba wa Bandari na AGL