
KWA kipindi cha miaka 4 ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan Hospitali ya Benjamini Mkapa imefanikiwa kupandikiza mimba kwa wanawake 21 huku wanaume 5 wakiwa wamewezeshwa kuwekewe vipandikizi maalumu kwenye uume. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea)
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Prof. Abel Makubi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Habari Maelezo Jijini Dodoma juu ya mafanikio miaka 4 ya uongozi wa Serikali iliyopo madarakani.
Prof. Makubi amesema kuwa katika kipindi cha miaka minne hospitali hiyo imeweza kuwahudumia wanawake 21 wenye kupandikizwa mimba ambapo waliohudumiwa ni kati ya miaka 35 hadi 50.
Amesema kuwa wahitaji hao ni wale ambao wamekuwa wakiangaika juu ya kupata mimba lakini hawakufanikiwa lakininwamekuwa nanuhitaji wa kupata watoto na wamekosa kwa njia ya kawaida.
Kwa upande wa wanaume ambao wamewezeshwa kupatiwa vipandikizi maalumu kwa kuhimalisha uume ni watano na hao ni wachache kutokana na tatizo la nguvu ya kiume kuwa kubwa lakini pia gharama ya matibabu kuwa kubwa zaidi.
Amesema gharama ya kuwekewa vipandikizi maalumu kwa ajili ya kuhimalisha nguvu za kiume ninkati ya Sh. 5 hadi 6 milioni.
Prof. Abel Makubi akizungumzia mafanikio ndani ya mika mitano ameeleza kuwa ni pamoja na uboreshaji na Kuongeza huduma za tiba za Kibingwa na Ubingwa wa Juu amesema kuwa ni pamoja nankuokoa kiasi cha Sh. 2.8 bilioni ambazo zingetumika kuwapatia rufaa wagonjwa ambao wangeenda hospitali za nje kupatiwa matibabu ya figo.
Amesema kuwa kwa sasa hospitali ya Benjamin Mkapa imekuwa ikitoa huduma ya upandikizaji figo pamoja kuvuna figo ambapo huduma hiyo ilikuwa ikipatiana nje ya nchi na sasa inapatikana nchini.
Ameeleza kuwa hospitali hiyo kwa kushirikiana na Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) zimekuwa zikitoa na kupanua huduma za tiba za kibingwa na Ubingwa wa juu wa Tiba na upasuaji kwa Wananchi mbalimbali wapatao million 14 kutoka mikoa zaidi ya 7 ya Tanzania.
Amesema kuwa katika kipindi cha miaka 4 Serikali imepanua huduma za kibingwa kutoka 14 hadi 20 na huduma za ubingwa wa juu kutoka 7 hadi 16.
Prof. Makubi amezitaja huduma hizo kuwa ni Upandikizaji figo (kidney transplant), upandikizaji uloto (Bone marrow transplant), upasuaji wa mishipa ya damu (cardiovascular surgery), upasuaji wa Moyo kwa kufungua kifua (cardiothoracic surgery), uvunjaji wa mawe kwenye mfumo wa mkojo kwa kutumia mawimbi (external shock wave and laser lithotripsy).
Huduma nyingine alizotaja kuwa ni pqmoja na upandikizaji uume(penile implantation), upasuaji wa ubongo na mfumo wa fahamu (neuro and spine surgery), upasuaji wa uti wa mgongo (spine surgery), kubadilisha nyonga na magoti (hip and knee replacement), upasuaji wa matundu madogo (laparoscopic and endoscopic surgery), Matibabu ya mfumo wa chakula (gastroenterology), Matibabu ya magonjwa ya figo (Nephrology).
Huduma nyingine ametaja kuwa ni uchujaji damu (Dialysis), Matibabu ya magonjwa ya Moyo (cardiology), uchunguzi na matibabu ya mishipa ya moyo kupitia maabara ya uchunguzi (catheterization laboratory), uchunguzi na matibabu ya kiradiolojia (interventional radiology),Tiba ya Magonjwa ya Hormone na kisukari(Endocrinology and Diabeteology) na Huduma za upandikizaji Mimba (IVF).
Huduma nyingine ni pamoja na kuimarishwa na kuboreshwa kwa huduma za upandikizaji figo.
Pia amesema kuwa Hospitali ya Benjamin Mkapa imefanikiwa kupandikiza figo wagonjwa 25 kati ya 50 kwa ndani ya miaka minne kwa gharama ya Sh. 875 milioni, kati ya hao wagonjwa 10 wamelipiwa matibabu haya kupitia mfuko maalum wa Samia Suluhu Hassan kwa kiasi cha Sh. 350 milioni.
ZINAZOFANANA
Sekta ya madini yapaisha pato la Taifa
Jamii yaaswa kufichua wafanyabishara za magendo Bagamoyo
Serikali ya Zanzibar yagoma kuvunja mkataba wa Bandari na AGL