February 24, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

TPA yataja miradi 10 ya kimkakati

Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Plasduce Mbossa

 

MKURUGENZI Kuu wa Mamlaka ya Bandari (TPA), Plasduce Mbossa amesema kuwa Serikali kupitia TPA inaendelea kutekeleza mapendekezo ya mpango kabambe ya maendeleo ya bandari nchini (2020 – 2045) na programu ya uboreshaji na uendeshaji wa bandari ambao ni mpango wa kitaifa. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Mpango huo ambao ulisajiliwa Oktoba, 2023 kwa jina la Tanzania Ports Development and Management Programme na kupewa namba ya mradi 4300.

Amesema kuwa katika Programu hiyo Serikali kupitia TPA imejipanga kutekeleza miradi 10 ya kimkakati ambayo ameitaja na kueleza kuwa itakuwa na tija kwa taifa na kwa ustawi wa Bandari.

Mbossa ameitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na Mradi wa kupokelea na kuhifadhia mafuta SRT ambapo utekelezaji wake umefikia asilimia 17 na unagharimu dola za kimarekani million 265.

Amesema kuwa mradi huo ukikamilika utapunguza siku za kuhudumia meli zenye ujazo wa 150,000 DWT kutoka siku kumi (10) mpaka tatu (3).

Ameutaja mradi mwingine ni Ujenzi wa kituo cha reli na mtandao wake ndani ya bandari ya Dar es Salaam na unagharimu dola za kimarekani million 119.955.

Amesema kuwa mradi huu ukikamilika utapunguza kiwango cha asilimia 98 cha shehena inayotoka bandarini kwa kutumia njia ya barabara na kupelekea kutatua tatizo la msongamano wa malori ndani na nje ya bandari.

Amesema kuwa ujenzi wa gati mbili zenye jumla ya urefu wa mita 500 ambao utagharimu dola za kimarekani million 250. Mradi huu ukikamilika utawezesha ufungaji wa meli mbili zenye ukubwa wa 50,000 DWT katika gati hizo kwa wakati mmoja.

Akiendelea kuelezea miradi hiyo ya bandari, Mbossa alisema kuwa hupo mradi wa ujenzi wa bandari maalum ya kisiwa – mgao mkoani Mtwara kwa ajili ya kuhudumia shehena chafu na utagharimu dola za kimarekani million 171.

Alisema kuwa mradi huo umelenga kuepusha athari za kimazingira na kuondoa changamoto zinazotokana na kuhudumia mizigo hii katika bandari ya Mtwara.

Akiutaja mradi wa tano, alisema ni pamoja na uboreshaji wa gati namba 8 hadi 11 yenye jumla za mita 720 pamoja na maeneo ya kuhifadhia makasha ambao utagharimu dola za kimarekani million 220 unaolenga kuimarisha huduma za kibandari.

Mkurugenzi huyo alieleza kuwa miradi mingine ni uendelezaji wa bandari kavu eneo la kurasini (Kurasini Logistics Centre) na Ihumwa – Dodoma miradi na miradi hiyo itagharimu dola za kimarekani million 157 na unaolenga kuongeza maeneo ya kufanyia shughuli za utekelezaji, uchakataji na kuhifadhi shehena kwa muda.

Akiendelea kutoa taarifa za maendeleo za TPA amesema kuwa hupo mradi wa uendelezaji wa bandari ya Kigoma utakaogharimu dola za kimarekani million 48.82.

Pia amesema mradi huo unalenga kuimarisha uchumi wa ushoroba wa kati. Ujenzi wa gati maalum la kuhudumia makasha na Gati la mafuta – Bandari ya Tanga utagarimu dola za kimarekani million 201.

“Mradi huu umelenga kuwa chachu ya maendeleo na ufunguo wa ushoroba wa Kaskazini.

“Ujenzi wa gati namba 12 hadi 15 utakao gharimu dola za kimarekani million 591.564 unaolenga kuongeza ufanisi wa bandari ya DSM.

“Ujenzi wa bandari mpya ya Mbegani Bagamoyo utakao gharimu dola za kimarekani billion 1.5.” ameeleza Mabossa.

About The Author

error: Content is protected !!