February 22, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Samia: Uhitaji wa kahawa duniani ni fursa kwa Afrika

 

RAIS wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema uhitaji wa kahawa Duniani ni fursa kubwa Barani Afrika ambako zao hili limegundulika. Anaripoti Apaikunda Mosha, Dar es Salaam … (endelea). 

Amezungumza haya katika Mkutano wa tatu wa nchi 25 Barani Afrika, zinazozalisha kahawa (G25 Coffee Summit), amesema takwimu zinaonyesha Dunia nzima watu bilion 3 wanakunywa vikombe vya kahawa kila siku, kati ya hivyo vipo vyenye kahawa nzuri inayozalishwa na wakulima wa Afrika na wengi wao wakiwa ni wakulima wadogo,” amesema Rais Samia.

Amesema kipindi cha nyuma kahawa yetu ilikuwa inaenda ulimwenguni inaongezwa thamani na kurudishwa kwetu na tunauziwa ghali, lakini sasa kumekuwa na ushindani wa uzalishaji na uengezaji wa thamani ya kahawa ndani ya Bara la Afrika.

Rais Samia amesema kuwa hatuna budi kuwapa nguvu vijana wetu ambao ameona wakitengenzeza kahawa pamoja na nakshi ya juu kama inavokuwa ya nchi kama Ujerumani, Uingereza na maeneo mengine, jambo ambalo linaonyesha hatua kubwa ambayo tumeifikia ndani ya Afrika.  

Aidha ameeleza ziara aliyofanya mkoani Ruvuma, September mwaka jana  alipotembelea shamba la  Kampuni ya AVIV, ameona ambavyo uongezaji wa thamani unavoweza kutoa fursa za ajira kwa vijana na wanawake wengi

Hata hivyo amesema kampuni ya  AVIV walivutiwa na mazingira mazuri ya uwekezaji hapa nchini na sasa wanalima na kuongeza thamani zaidi ya tani 200 za kahawa ya Arabica na wanaajiri watu zaidi ya 4,000 ikiwemo ajira za msimu wakati wa kupanda na kuvuna.

Mwisho, Rais Samia amesema amefurahishwa kufanyika kwa mkutano huu wa tatu wa nchi zinazozalisha kahawa Barani Afrika, wenye kauli mbiu inayosema “fungua fursa za ajira kwa vijana kupitia uhimarishaji wa kahawa  Barani Afrika.”

About The Author

error: Content is protected !!