
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. Emmanuel Nchimbi
KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. Emmanuel Nchimbi amewatangazia kiama wanachama wa chama hicho ambao wanataka kugombea nafasi mbalimbali kwa kutoa matamko ya kutaka kuwa wagombea pekee. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).
Balozi Dk. Nchimbi amesema kuwa wapo baadhi ya wanachama ambao kwa sasa wameanzisha tamaduni ya kutengeneza makundi ya kutoa matamko ya kuwataka baadhi ya wanasiasa ndani ya chama hicho kuwa wagombea pekee jambo ambalo halikubaliki ndani ya chama na wanachama wa aina hiyo watakatwa mapema majina yao.
Kiongozi huyo wa juu katika chama ametoa rai hiyo leo tarehe 19 Februari 2025 alipokuwa akifungua mafunzo kwa makatibu tawi, kata, wilaya na mkoa katika mkoa wa Dodoma yaliyofanyika jijini Dodoma leo.
“Wapo wanachama watakao gombea na watakao hamasisha matamkoa kwenye maeneo yao ili wawe wagombea pekee wagombea hao watahamasisha kuenguliwa kwa majina yao kirahisi.
“Pia wapowagombea ambao wameanzisha utaratibu wa kutengeneza makundi ya kutoa matamko mbalimbali ya kulazimisha asijitokeze mgombea mwingine kuwania nafasi furani ya uchaguzi,na wengine wanatengeneza sherehe za kumbukizi ya kuzaliwa kwa bini yake na kuwaharika wana CCM na kuwalipa posho huku wakiwa wamevalua nguo za kijani, watu wa aina hiyo watakatwa majina yao mapema na wala wasidhani kuwa wataonewa huruma,” ameeleza Dk. Nchimbi.
Ameeleza kuwa kuna mchezo wa mtu kuandaa sherehe ya kufanya kumbukizi ya ndoa kwa kutimiza miaka 5 wakati ndoa ina miaka 3 na anakuwa na ujasiri wa kuharika wana CCM 300 na kuwalipa posho jambo abalo linaonesha wazi kuwa hatua hiyo ni ushawishi wa rushwa.
Kiongozi huyo amesema kuwa kutokana nankuwepo kwa matukio hayo uongozi wa CCM umeanza kufuatilia matukio ya aina hiyo na iwapo uongozi utajiridhisha kuwa kuna mgombea anafanya vitendo vya kutoa rushwa au kusingizia kufanya sherehe na matamko mgombea huyo hataweza kupenya.
Dk. Nchimbi amewataka makatibu ambao watakuwa sehemu ya usimamizi wa uchauzi uhakikisha wanafuatilia matukio na uweka rekodi vizuri ili pale itakapo bainika kutokea mambo hayo atakayekuwa anagombea achujwe mapema.
Katika hatua nyingine amesema kuwa uchaguzi ndani ya chama hicho unalenga kuwasimamisha wagombea ambao wanakubalika katika jamii na soyo wale ambao wanaingia madarakani kwa kutoa rushwa.
“Kuna watu wanatenga laki tano tano na kuwahesabu wajumbe 300 kwa kuwaonga na wanapopata uongozi wanakuwa hawafanyi kitu chochote kwa madai kuwa wao walimaliza mchezo kwa kuwanunua.
“Wote mnajua kuwa uchaguzi unaweza kuwa mgumu kulingana na watu mliowachagua na tabia zao,mlevi anaweza kupita barabarani anayumba lakini hakuna wa kumsema lakini ukiwa umevaa sare yako ya chama na ukaonekana umelewa utapigwa picha na kuwekwa mitandaoni na kuanza kueleza kuwa kigogo wa CCM akutwa amelewa chakali,” ameeleza Dk. Nchimbi.
Aidha Dk. Nchimbi amesema kuwa kwa sasa chama kinataka kupata viongozi makini na wachapa kazi ambao watakuwa kinyume na masuala ya rushwa sambamba na kutokuchafuana kati ya waliopo madarakani na wale wanaotaka kuingia.
ZINAZOFANANA
Gambo awashukia wanaopinga uteuzi wa Samia
Mkuu wa mkoa Mwanza aitisha kikao kumsaka kada wa Chadema
DCEA yateketeza ekari 336 za mashamba ya bangi Kondoa