
Katibu wa Baraza la Vijana Chadema Mkoa wa Mwanza, Amani Manengelo
MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda ameitisha kikao ili kupanga jitihada za pamoja za kumsaka Katibu wa Baraza la Vijana Chadema Mkoa wa Mwanza, Amani Manengelo anayedaiwa kutekwa Ijumaa ya wiki iliyopita. Anaripoti Mwandishi Wetu. Mwanza … (endelea).
Akiwa Jijini Mwanza leo tarehe 18 February 2025 wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya msaada wa kisheria ya Mama Samia Mkoani Mwanza, Mtanda ameitisha kikao kati yake na kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza, Familia ya Katibu wa Baraza la Vijana Chadema Mkoa wa Mwanza pamoja na Uongozi wa Chadema Mkoa wa Mwanza ili kupanga jitihada za pamoja za kumsaka Ndugu Manengelo.
Aidha, kufuatia taarifa hizo zilizotolewa na kuchapishwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo ya wanachama na wafuasi wa Chadema zinazoeleza kuwa Manengelo ametekwa na watu wanaodaiwa kuwa ni maafisa wa Jeshi la Polisi.

Mtanda amekanusha madai hayo akisisitiza serikali ya awamu ya sita ya Rais Samia Suluhu Hassan haijawahi na haina mpango wa kumteka mtu yeyote yule, awe CHADEMA au mfanyabiashara kwa sababu serikali haina ugomvi na yeyote.
Amesema kuwa amepata taarifa kuwa Vijana wa Chadema (BAVICHA) wamepanga kukusanyika kesho mapema ofisini kwake kushinikiza kuelezwa alipo kiongozi wao anayedaiwa kutekwa.
“Ninawakaribisha hii ni serikali yenu, mwananchi yeyote anapokuwa na kero yake anakaribishwa ndani ya serikali. Tahadhari yangu mje vizuri ili muondoke vizuri, kwangu unavyokuja ndivyo utakavyopokelewa na utakavyohudumiwa,” amesema Mtanda.
ZINAZOFANANA
SBL yazindua kampeni ya SMASHED kukabiliana na unywaji wa pombe chini ya umri
DAWASA wajitia kitanzi changamoto za maji Temeke
Uingereza yafurahishwa na maboresho Bandari ya Dar, yaipongeza serikali