
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Majaliwa
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema mnufaika wa mkopo atatakiwa kulipa kiasi cha fedha aliyopewa tu kwani Tozo zimeondolewa na Serikali kwa sababu zilikuwa zinaongeza kiasi cha madeni ya mikopo hiyo na kufanya wakopaji washindwe kurejesha. Anaripoti Apaikunda Mosha, Dar es Salaam … (endelea).
Ameyasema haya leo tarehe 17 Februari 2025, katika kilele cha Maadhimisho ya miaka 20 ya Bodi ya mkopo ya wanafunzi wa Elimu ya juu, yaliyoanza tangu tarehe 10 Februari 2025, yaliyoambatana na huduma za kliniki, Makala mbalimbali na mbio za marathoni.
Akizungumzia kwa kina mafanikio makubwa ambayo yameletwa na taasisi ya mikopo kwa jamii yetu amesema licha ya Changamoto ambayo bodi hii imepitia, lakini imefanikiwa kuongeza Wigo wa upatikanaji wa Elimu ya juu apa nchini kwa vijana wengi.
“Kauli mbiu hii ya ‘Athari chanya, ubunifu na huduma’ imebeba uhalisia, na mahitaji halisi ya jamii yetu kwani sasa athari chanya ni matarajio kwa kila afua inayowekezwa hapa nchini na suala la ubunifu ni muhimu sana katika kuimarisha suala la utoaji wa huduma.” amesema.
Ameainisha namna ambavyo mkopo huu umewezesha wanafunzi 830,000 tangu kuanzishwa kwa Bodi hii, aidha fedha za kitanzania Sh. 8.2 trilioni zimetumika katika kugharamia mafunzo ya wanafunzi wa Elimu ya juu.
Majaliwa ameipongeza Bodi kwa na mfumo wa kidigitali, jambo linalofanya taasisi hii iendane na mfumo wa kasi wa teknolojia, pia wameweza kufanikiwa kukusanya fedha kiasi cha Sh. 1.5 trilioni kutoka kwa wanafufaika wa mkopo ikiwa ni sehemu ya kiasi cha Sh. 2.9 trilioni zilizoiva zinazotakiwa kurejeshwa.
Aidha, Waziri amesema kuwa Bodi ya Mkopo ni miongoni mwa taasisi bora kabisa za serikali barani Afrika kutokana na mafanikio makubwa iliyopata ya kusimamia utoaji na urejeshwaji wa mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya juu.
Mwisho ameitaka Bodi ya mkopo na wadau kuongeza wigo wa utoaji wa elimu kuhusu vigezo vinavowawezesha wanufaika kupata mkopo na kupitia shule zote za kidato cha tano na sita ili kuonyesha namna nzuri ambayo wanaweza kuomba mikopo hiyo.
ZINAZOFANANA
SBL yazindua kampeni ya SMASHED kukabiliana na unywaji wa pombe chini ya umri
DAWASA wajitia kitanzi changamoto za maji Temeke
Sekretarieti ya Ajira yatoa ufafanuzi ajira za walimu