![](https://mwanahalisionline.com/wp-content/uploads/2025/02/1733397471215.jpg)
Dk. Ntuli Kapologwe
MKURUGENZI wa Kinga Wizara ya Afya, Dk. Ntuli Kapologwe, ameshinda nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Jumuiya ya Afya ya Nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini (ECSA – HC) Tanzania imepata nafasi hii baaada ya miaka 27. Anaripoti Apaikunda Mosha, Dar es Salaam … (endelea).
Zoezi la uchaguzi huo limehitimishwa leo tarehe 12 Februari 2025, ambapo jumla ya Waombaji 47 waliwasilisha wasifu wao na kati yao, saba walichaguliwa kuendelea baada ya mchujo wa awali.
Akizungumza baada ya tukio hilo Waziri Mhagama amesema mara baada ya usaili uliofanywa na Kamati ya Mkutano wa Makatibu wakuu wa nchi na wanachama Dk. Ntuli Kapologwe alipata alama za juu zaidi na kuingia katika hatua ya mwisho pamoja na wagombea wengine wawili kutoka Kenya na Malawi.
Amesema Tanzania haya ni mafanikio makubwa sana kwa nchi yetu, kwani awamu hii ni ya pili kwa kipindi cha miaka 51 cha Jumuiya hii, baada ya kupata nafasi hiyo alipohudumu Dk. Winny Mpanju mwaka 1983 na 2000.
Hata hivyo, Dk. Ntuli anachukua nafasi hiyo kutoka kwa Prof. Yoswa Dambisya wa Uganda ambaye amehudumu kwenye nafasi hiyo kwa mihula miwili ndani ya miaka 10.
Aidha kwa kuzingatia vigezo maalum vilivyowekwa katika makubaliano ya Jumuiya hiyo, Dk.Ntuli ataongoza kwa muda wa miaka mitano.
ZINAZOFANANA
CCM yamfukuza aliyepinga uteuzi wa Rais Samia kugombea
Namibia wamlilia Sam Nujoma
ACT-Wazalendo chaunda Kamati ya Ilani