![](https://mwanahalisionline.com/wp-content/uploads/2025/02/427997228_794761879345617_7060279533741175851_n.jpg)
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TCRA, Jones Kilimbe
IMEELEZWA kuwa usalama wa matumizi ya mtandao na kuhimarishwa vyema kwa matumizi bora na yenye faida ni wazi kuwa amani ya Nchi na mtu binafusi itakuwepo kwa kiwango kikubwa. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Jones Kilimbe, wakati wa Maadhimisho ya siku ya Usalama Mtandaoni 2025 yaliyofanyika Jijini Dodoma kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo walimu wa shule ya msingi,vyuo vya kati na vyuo vya elimu ya juu.
Akifungua maadhimisho hayo amesema kuwa ili kuwa na taifa lenye watu bora kimaadili na kiuchumi ni bora kutumia vyema mitandao kwa matumizi bora na yenye manufaa kwa jamii pamoja na taifa kwa ujumla.
Akiendelea kuzungumza na wadau mbalimbali wa matumizi ya mtandao amesema kuwa kwa sasa kuna urahisi mkubwa matumìzi ya kimtandao pamoja na hasara kubwa iwapo mitandao itatumiwa vibaya.
Akizungumzia masomo ya sayansi kwa wanafunzi amewataka kutoogopa masomo ya sayansi na hesabu kwa kuwa siyo magumu kama inavyoelezeka.
“Ninyi wanafunzi mnaosoma msiogope masomo ya Sayansi na Hesabu kwani ni masomo pekee ambayo hanafanana duniani kote hivyo hayabadiliki na unaweza kuyapata mahali popote na kukufanya kuajiliwa mahali popote,” ameeleza Mwenyekiti wa Bodi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Leseni na Ufuatiliaji kutoka TCRA, John Dafa amesema kuwa siku ya usalama mtandaoni uadhimishwa jumanne ya pili ya mwezi Februari kila mwaka ambayo ni mpango wa kimataifa ulioanzishwa mwaka 2004 kwa lengo la kuhamasisha matumizi sahihi na salama ya mtandao wa intaneti.
“Siku hii inasheherekewa takribani katika nchi 190 duniani,vilevile maadhimisho haya yanaunganisha mabilioni ya watu ulimwenguni kuhamasisha matumizi sahihi na salama mtandaoni nakuongeza uelewa kuhusu masuala ya mtambuka mtandaoni haya miongoni mwa fursa yanayotokana na matumizi hayo,
“Huu ni mwaka wa 21 toka mtandao huu uanzishwe tangu mkakati huu wa Safer Internet yanayokwenda na Kaulimbiu ya maadhimisho ya mwaka huu “Jilinde wewe na uwapendao dhidi ya ulaghai uhalifu mtandaoni,” amesema.
Dafa amesema Kauli mbiu hiyo inatukumbusha umuhimu wa kuongeza umakini kwa kutumia mitandao na mifumo ya teknolojia katika dhama hizi za taarifa(Information society)ambapo matumizi ya teknolojia yakumbana na changamoto za wingi wa uangalifu mtandaoni hawa wanatumia mbinu mbalimbali zikiwemo zinazovutia nakushawishi.
Kwa upande wa mwanafunzi wa Chuo cha Biashara CBE, Janeth Butashobya amesema kuwa utumiaji wa mitandao kwa sasa umestawisha upatikanaji wa nyenzo mbalimbali za kusaidia kujisomea.
Pia amesema kuwa upatikanaji wa mitandao kwa maana ya matumizi ya Intaneti kumerahisisha upatikanajinwa huduma muhimu na kupunguza matumizi matumizi ya muda.
ZINAZOFANANA
Dk. Mpango mgeni rasmi kikao kazi cha Serikali mtandao
Waziri Chana afungua rasmi onyesha la wiki ya Ubunifu wa Italia
mapambano dhidi ya biashara haramu ya maliasili yazidi kuimarishwa