March 13, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Tanzania yapewa uenyeji mkutano wa kikanda Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Afrika

 

TANZANIA imeendelea kushiriki na kuandaa mikutano ya kimataifa kwa mara nyingine tena baada ya kupewa uenyeji wa mkutano wa kikanda wa mamlaka ya viwanja vya ndege utakaofanyika jiji la Arusha. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea). 

Hii ni shughuli kubwa nyingine Tanzania imekabidhiwa kuandaa mkutano wa kikanda wa mamlaka ya viwanja vya ndege ikiwa ni kwa mara ya pili baada ya ule wa mara ya kwanza uliofanyika mwaka 2007.

Tanzania imeendelea kupewa sifa hii ya kuandaa mkutano wa viwanja vyote vya ndege Afrika kwa kuangalia usalama wa abiria, huduma bora na usalama pamoja na idadi ya ndege zinazotua Tanzania na kuvipiku viwanja vingine vikubwa barani Afrika.

Katika awamu hii ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, Tanzania imekuwa ikiheshimika na kusikilizwa sana na mataifa ya Afrika na wakati mwingine kuchaguliwa kama eneo la kujadili masuala muhimu kama ya amani na upatanisho pamoja na mijadala mikubwa inayoamua mustakabali wa bara la Afrika.

Kwa takribani wiki mbili za mwezi January na Febryary ya mwaka 2025 Tanzania imeshiriki kuandaa mikutano miwili mikubwa ikiwemo mkutano wa Nishati pamoja na ule mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ulio unganishwa na mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Afrika Mashariki kujadili amani masharriki ya Congo.

Kwa Mikutano hii inaonyesha jukumu la Tanzania na umuhimu wake katika diplomasia na masuala ya kimataifa ikiwa ni njia mojawapo ya kuchechemua uchumi wa Taifa.

About The Author

error: Content is protected !!