February 5, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Ndoa ya Ramovic na Yanga yavunjika baada ya siku 80

 

KLABU ya soka ya Yanga imetangaza kufikia makubaliano ya pande zote mbili na aliyekuwa kocha wao mkuu, Sead Ramovic mara baada ya kuhudumu kwenye klabu hiyo kwa siku 80. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Ramovic alitambulishwa rasmi na Yanga tarehe 15 Novemba 2024, akichukua nafasi ya Miguel Gamond ambaye alifungashiwa virago kufuatia matokeo mabaya ya timu hiyo.

Kwenye taarifa yao iliyotoka hii leo tarehe 04 Februari 2025, imeeleza kuwa nafasi ya Ramovic itachukuliwa na Miloud Hamdi.

Hamdi anakuwa kocha wa tatu kuhudumu ndani ya klabu hiyo tangu kuanza kwa msimu huu wa 2024/25, alitokea klabu ya Singida Black Star yenye makao yake mkoani Singida.

Ramovic ameachana na klabu hiyo, huku baadhi ya taarifa zikieleza kuwa amepata ofa kwenye moja ya timu nchi Algeria ambayo atajiunga nayo hivi karibu.

Wakati Yanga ikiachana na kocha huyo, kesho itashuka dimbani kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya KenGold kutoka Mbeya, mchezo utakopigwa kwenye Uwanja wa KMC Complex majira ya saa 10 jioni.

About The Author

error: Content is protected !!