
MARAIS wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), wanatarajia kukutana Jumamosi tarehe 8 Februari jijini Dar es Salaam kujadili mgogoro unaoendelea Mashariki ya Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo DRC huku Rais wa nchi hiyo Felix Tshisekedi na Rais wa Rwanda Paul Kagame wakithibitisha kuhudhuria. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).
Taarifa hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Rais wa Kenya William Ruto jana tarehe 3 Februari 2025.
Ruto alisema kuwa Mwenyeji wa Mkutano huo Rais wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan ameridhia kuwa mwenyeji wa mkutano huo wenye lengo la kumaliza mgogoro huo.
Mkutano huo utakaotanguliwa na mkutano wa Mawaziri wa Jumuiya hiyo tarehe 7 Februari.
Rais Ruto alisema kuwa Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, Rais wa Uganda Yoweri Museveni na Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamod.
ZINAZOFANANA
Mtanzania achaguliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Jumuiya ya Afya ya Nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini
Waziri Chana afungua rasmi onyesha la wiki ya Ubunifu wa Italia
CCM yamfukuza aliyepinga uteuzi wa Rais Samia kugombea