January 31, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Madeleka ataka maridhiano yatumike kesi ya Dk. Slaa

Wakili Peter Madeleka

 

WAKILI Peter Madeleka ameomba kutumika kwa njia ya maridhiano kwenye kesi ya Dk. Wilbrod Slaa, kutokana na kuonekana kwa juhudi za makusudi za kukwamisha haki ya mshtakiwa huyo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea)

Madeleka ameyasema hayo nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mara baada ya shauri hilo kuahirishwa kwa Saa 2 kufuatia mabishano makali ya kisheria kutoka kwa mawakili wa pande zote mbili.

Madeleka amesema kuwa, ameamua kusema hivyo kama endapo njia za kimahakama za utoaji haki kishindikana, kwa kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia kwa Makamu Mwenyekiti wake Bara, Stephen Wassira wamefungua milango kwa mtu yoyote kufanya maridhiano nao.

“Naomba nimpongeze Stephen Wassira, ambaye ni makamu Mwenyekiti wa CCM Bara kwa kuutangazia umma kwamba CCM ipo tayari kufanya maridhiano na mtu mwengine yoyote, nayasema haya kwa sababu njia za kimahakama zinaonenekana zitashindikana kupata haki ya Dk. Slaa,” alisema Madeleka

Hayo yote yemekuja kufuatia Mawakili wa upande wa Serikali kuweka zuio kwenye mahakama ya Kisutu kusomwa kwa uamuzi wa dhamana, na kusema kuwa wamejipanga kukayakatia rufaa maamuzi ya Mahakama Kuu yaliyotoka jana.

Maamuzi ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam hapo jana, yaliamuru kesi hiyo irejee kwenye mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu na uamuzi kuhusu dhamana ya Dk. Slaa utolewe kwa haraka.

Zuio hilo kuhusu Mahakama hiyo kutotakiwa kutoa uamuzi wa dhamana, lilipingwa vikali na upande wa utetezi na kufanya hakimu kuahirisha shauri hilo mpaka Saa 9 jioni, kuja kutoa uamuzi mdogo wa kama wataendelea na uamuzi wa dhamana au watasubili kusikiliza rufaa

About The Author

error: Content is protected !!