January 30, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Wanawake vyombo vya ulinzi na usalama Songwe kushiriki Siku ya Wanawake Duniani

Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake Mkoa wa Songwe (TPF- NET) Mkoa wa Songwe Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Akama Shaaban

 

ASKARI wa kike kutoka Vyombo vya Ulinzi na Usalama mkoani Songwe waungana ili kushiriki kikamilifu katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake  Duniani itakayofanyika Machi 2025. Anaripoti Issa Mwadangala, Songwe … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa Januari 30, 2025 na Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake Mkoa wa Songwe (TPF- NET) Mkoa wa Songwe Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Akama Shaaban Katika mkutano na Wawakilishi wa Vyombo hivyo.

ACP Akama alisema, wakati dunia ikiendelea kuhamasisha Usawa wa kijinsia kupitia Mpango wa Maendeleo endelevu (SDG’s 2030) lengo namba 5 pamoja na Mikataba mbalimbali ya Kimataifa, Wanawake wa Vyombo hivyo hawana budi kushiriki kikamilifu katika siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani inayoadhimishwa tarehe 8 Machi kila Mwaka duniani kote.

Katika kikao hicho alielezea umuhimu wa siku hiyo ambayo inalenga kuunga mkono harakati zinazofanywa na mashirika mbalimbali ya kimataifa katika kumuwezesha mwanamke kwenye nafasi za uongozi, uchumi na maamuzi ikiwa ni pamoja na kuambatana na shughuli mbalimbali ikiwemo kutoa elimu kwa jamii na kutoa misaada kwa makundi maalumu

Kikao hicho cha Maandalizi ya kuelekea siku ya maadhimisho ya kilele cha Wanawake Duniani kilichofanyika katika ukumbi wa Polisi Vwawa Wilaya ya Mbozi kilishirikisha Jeshi la Polisi, Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Magereza, Zimamoto na Uhamiaji.

About The Author

error: Content is protected !!