KATIKA uboreshaji sekta ya elimu nchini na kuifanya elimu ya Tanzania kuwa ya kiwango cha juu na ufahamu mkubwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Samia Suluhu Hasani anatarajia kufanya Uzinduzi wa sera ya Elimu na madunzo ya mwaka 2024 toleo la 2023 na mitaala iliyoboreshwa kuzinduliwa rasm 31 Januari 2025. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).
Akizungumzia uzinduzi huo msemaji wa Serikali Greison Msigwa amesema kuwa Serikali inatambua wazi kuwa watu ndiyo nguvu kazi hivyo ni muhimu kuboresha elimu na mitaala kuanzia ngazi ya shule za awali hadi elimu ya juu.
Amesema utekelezaji wa elimu ya mafunzo ya mwaka 2024 na toleo la mwaka 2023 kutakuwepo na uzinduzi ambao utawezesha kuzindua sera hiyo ambayo ni muhimu na ya kihistoria.
Msigwa amesema kuwa sera ilichukua muda mrefu bila kutekelezwa lakini kufuatia utendaji wa rais Samia amefanikisha utekelezaji wa sera hiyo ambayo itawezesha kupata vijana wenye elimu ya ujuzi na uzalendo zaidi.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknologia Prof. Carolyne Nombo amesema kuwa ili kupata taifa lenye watu makini ni lazima upate watu wenye elimu ikiwa ni pamoja na suala zima la kuwapata watu wwnye elimu ya ufundi stadi.
Hata hivyo amesema kuwa kwa sasa ni lazima kuwa na watu ambao wanaendana na suala zima la mabadiliko ya teknolojia ambao wataweza kupambana na wakati.
Kutokana na umuhimu wa elimu nchini ni wazi kila mtanzania akatambua kuwa ni vyema kuelewa umuhimu wa sera na elimu iliyoboreshwa kwa faida ya watabzania huku akieleza kuwa ipo mihongozo muhimu ambayo itawezesha kuboresha elimu kuanzia ngazi ya elimu ya Awali ,shuke ya msingi darasa la kwanza hadi la sita na elimu ya juu.
Kutokana na tukio hilo muhimu watanzania wote wametakiwa kuhakikisha wanafuatilia uzinduzi wa sera hiyo kwa nia ya kujua nini umuhimu wa sera hiyo.
ZINAZOFANANA
Wazazi walalamikia walimu Ilala, kisa chakula cha shule
FEZA Boys yafaulisha wanafunzi wote
NECTA watangaza matokeo ya kidato cha nne