BENK ya Ushirika ya Kidijitali Tanzania imetaja mambo makubwa matatu ambayo yataifanya benki hiyo kuwa tofauti na benki nyingine tanzania huku ikielezwa ni benki mahususi kwa ukombozi wa mkulima,mfuhaji na watu wa kada ya chini. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).
Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya Ushirika, Godfrey Ng’urah akitoa maelezo ya uanzoshwaji na umuhimu wa benki hiyo kwa wadau mbalimbali wa Benki hiyo na waandishi wa habari amesema kuwa benki inalenga kuwafikia watu wengi zaidi pamoja na utoaji huduma bora na kwa haraka kwa kutumia mifumo ya kidigitali zaidi.
Akitoa taarifa fupi juu ya utendaji wa kazi na utoaji wa huduma ya benki hiyo amesema kuwa dira yake ni kuhakikisha kuwa inakuwa benki kiongozi ya kidijitali nchini na kuchochea kwa kasi kubwa ujumuishi wa huduma za kibenki na kifedha.
Mkurugenzi huyo amezidi kueleza kuwa dhima ya benki hiyo ni pamoja kufanya kazi kwa njia ya Kiteknolojia na huduma bora za kibenki kidijitali na kuwafikia watanzania wengi kwa mara moja kwa urahisi,wepesi na kwa gharama nafuu.
Katika kuendelea kuelezea utendaji wa kazi na utoaji wa huduma katika benki hiyo Mkurugenzi Mtendaji N’gurah amesema Adhma ya benki hiyo pia ni kuchochea mapinduzi ya kiuchumi na kijamii kwa nguvu ya TEHAMA ili kuleta ustawi kwa watu wote wa kwa ngazi zote.
Akielezea uwepo wa benki ya Ushirika Tanzania (Coop Bank) Mkurugenzi mtendaji N’gurah amesema kuwa benki hiyo inalenga kutumia rasilimali na fedha za wanahisa kufanya mapinduzi makubwa katika sekta ya kifedha hapa nchini kwa kulenga asilimia 78 ya watanzania wasiokuwa na huduma za kibenki na kutumia masoko mama la Ushirika kufikia vyama 10,000 vyenye wanachama au wateja zaidi ya milioni 10 kote nchini.
“Kwa kuwekeza kwenye TEHAMA ikichagizwa na uwepo na msukumo mkubwa wa kiserikali kujenga uchumi wa kidijitali na uwepo wa msukumo mkubwa wa kiserikali kujenga uchumi wa kidijitali.
“Tutafanya uwekezaji mkubwa katika mifumo ya kutoa huduma za kibenki kidijitali ikiwa ni pamoja na mfumo mama wa kibenki (SBS) Mifumo ya kiakili bandia (Akili mnemba) mifumo ya utambuzi na kupata taarifa za wateja na mazoea yao .
“Mifumo mingine ni utunzaji wa kazi data hewani,huduma za kibenki zilizojengwa juu ya shughuli za kidigitali na uchumi ya takwimu,huduma za kibenki kwa simu na huduma za kibenki kwa mawakala”ameeleza Mkurugenzi Mtendaji Ng’urah.
Katika taarifa yake pia ameeleza kuwa Benki ya Ushirika Tanzania (Coop Bank)kwa sasa inamilikiwa na wanaushirika kama wawekezaji wakuu na baadhi ya wawekezaji kimkakati kama vile vyama vya ushirika asilimia 51,Beki ya CRDB asilimia 20, Taasisi na watu binafsi asilimia 19 na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania asilimia 10.
Mageuzi ya kimkakati na viashiria vya mafanikio 2020-2024
Mkurugenzi Mtendaji ameeleza kuwa katika kipindi cha miaka minne ya mageuzi ya benki zote mbili ilizounda Benki ya Ushirika- Coop BANK, Benki imeongeza wigo wa bidhaa zake sokoni ikiwa ni pamoja na akaunti mahusisi kwa wajasiriamali, vijana na wanawake, mikopo ya Bajaji na pikipiki kwa vijana, Akaunti maalum ya Kilimo kwa wakulima isiyo na makato.
Aidha, Benki imekuza na kuongeza idadi ya wateja na akaunti zake kufikia wateja Elfu 33, mwaka 2024 toka wateja Elfu Elf 6 mwaka 2020.
Amwendelea kueleza kuwa uendeshaji umezidi kuimarika kwa tija na ufanisi mkubwa huku faida ya Benki ikikua kutoka hasara ya shilingi milioni mia sita thelathini (630 m) mwaka 2020, hadi kufikia faida ya shilingi milioni mianane na tisini na moja (891mn) kabla ya kodi sawa na ongezeko la Faida kwa zaidi ya asilimia 241 katika kipindi kifupi cha miaka 4.
Hali kadhalika, Mtaji na fedha za wanahisa umekuwa toka shilingi bilioni 3.7Bn ya mwaka 2020, hadi kufikia shilingi bilioni 27.4 mwaka 2024, sawa na ukuaji wa asilimia 640% ndani ya miaka 4. Ahsanteni sana wana ushirika,wateja, na wadau wetu wote, tusingeliweza bila ninyi.
ZINAZOFANANA
Dk. Biteko aongoza waombolezaji kuaga miili ya wanafunzi waliokufa kwa radi
Wanawake vyombo vya ulinzi na usalama Songwe kushiriki Siku ya Wanawake Duniani
Ofisi ya Makamu wa Rais yaandaa mkakati wa usimamizi wa taka