BAADHI ya wazazi katika Kata ya Kivule Ilala jijijni wametupia lawama shule ya msingi Anex, Serengeti na Kivule Kwa kuwatenga, kuwanyanyapaa wanafunzi ambao wazazi wao wameshindwa kuchangia shilingi ,1500 ya gharama ya chakula na masomo ya ziada katika shule hiizo. Anaripoti Mary Victior, Dar es Salaam … (endelea).
Wakizungumza kwa sharti ya kutotajwa majina gazetini , kwa nyakati tofauti wazazi hao walisema watoto wao wamekuwa wakiwaletea malalamiko ya kutengwa shuleni kwa kushindwa kuchangia gharama ya chakula na huduma ya masomo ya ziada yanayoyolewa katika shule hizo .
“Wali wenyewe unaopikwa umeuona? Mtoto akikata tonge tatu tu kamaliza , na sio ombi ni lazima kuchangia gharama hizo. Kwa mfano mimi nina watoto sita, ninalazimika kugharamia 6000 kila siku huduma hizo. Hapo bado sijaweka nauli na huduma nyingine.
“‘Nikipata nitalipa, nikikosa wakacheze tu, mara walimishwe. Maana 6000 si pesa ya kuwa nayo kila siku, na usipolipa ndio unakuwa uhasama kwa walimu. Kama hujampa hela mwanao hata daftari lake halishahihishwi wala hawamkohoi, wanawatenga kabisa na wenzao, wanaishi kinyonge shuleni”alisema mmoja wa wazazi
Mwenyekiti wa Kamati ya Wazazi Shule ya Msingi Serengeti Bihimba Nassoro alikiri kuwepo kwa changamoto hizo akisema suala la waraka wa serikali imetaka watoto wale shuleni, kila mtoto atampatia mtoto wake kiasi cha shilingi 200 kwa ajili ya uji na pia shilingi 500 Kwa ajili ya chakula ikiwemo pia masomo ya ziada shilingi 200.
Akitolea mfano Shule ya Serengeti Bihimba alisema, ina watoto zaidi ya 2000, walimu wa kuajiriwa hata 30 hawafiki, ili kuziba pengo shule imejipa utaratibu wa kutafuta walimu nje ya mfumo; “Kuna walimu tumewapata 10 wa kujitolea, nilikwenda kuonana na mkurugenzi wa Iala nikamwambia shule za msingi tuna uhaba wa walimu, tumepata walimu wa kujitolea lakini mimi na mwalimu wangu mkuu hatuna vyanzo vya fedha za kuwalipa, mkurugenzi akashauri turudi kwenye kamati za shule tutafute vyanzo vya mapato.”
Kwa mujibu wa Bihimba katika kikao cha wazazi kilichofanyika mapema mwaka jana, kila mwalimu wa kujitolea aliomba alipwe Sh. 400,000. Nikawauliza wazazi, nao wakagoma
“Ninachokiona Mimi Serikali haitaki kusimamia ukweli, ukishindwa kusimamia ukweli unatengeneza bomu, shule nyingi za sekondari na msingi hazina walimu . Mkurugenzi na afisa wanakwambia fedha ya kuajiri walimu.
“Katika kuchangia miundombinu kielimu nimejitolea mifuko 20 ya sementi, nilitoa mchango wangu huo katika mahafali ya darasa la saba mwaka jana. Nikatoa tena vifaa vya Tehama kompyuta na mashine ya photocopy, vyote vina gharama ya shilingi 1,000,000. Nilikwenda na mkuu wangu wa shule Kariakoo nikamwambia achague, nimefanya hivyo ukizingatia hatulipwi hata posho kwenye majukumu yetu ya kusimamia shule hizi, ilihali mkurugenzi manispaa analipwa mshahara, nyumba ya kuishi bure, gari bure, chakula bure, anashinda ofisini na hatujawahi hata kumuona katika shule yoyote huku Kivule.
“Nimalizie kwa kusisitiza kwamba wazazi wanaohudhuria vikao vya kamati za shule suala la kuchanga chakula shuleni wanajua, wasiojua ni wale ambao hawahudhurii vikao”alisema Bihimba
Aliyekuwa Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Ilala, Mwalimu Hossein Mghewa alisema; Bahati mbaya nimehama Manispaa ya Ilala wazazi kuchangia huduma ya chakula ni suala la lazima, wao wanalalamika nini?
Naye, Afisa Habari wa Manispaa ya Ilala, Tabu Shaibu alisema atayafikisha malalamiko yaliyoibuliwa kwa wahusika.
“Nayafikisha kwa wahusika, kwa kuwa ni malalamiko nitayafikisha kwa wahusika waweze kuyafanyia kazi,” alisema Tabu.
ZINAZOFANANA
FEZA Boys yafaulisha wanafunzi wote
NECTA watangaza matokeo ya kidato cha nne
Waziri Jafo akagua maandalizi miaka 60 ya CBE