January 27, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Waziri Mhagama: Tumejiandaa kuwahudumia wageni katika sekta ya afya

 

WIZARA ya Afya nchini imesema kuwa imechukua tahadhali zote zinazohusu masuala ya afya kwa ajili ya kuwahudumia viongozi na wageni mbalimbali watakaohudhuria Mkutano Mkuu wa Nishati Barani Afrika utakaoanza kesho tarehe 27 Januari 2025. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza leo 26 Januari 2025, kwenye Hospitali ya Agha Khan ikiwa ni ziara ya ukaguzi wa hospitali mbalimbali zilizoandaliwa kwa ajili ya kuhudumia wageni hao, Waziri wa Afya, Jenister Mhagama amesema nchi imejianda vizuri katika eneo hilo kwa ajili ya kuwahudumia wageni watakaopata dharula kiafya.

“Kama tunavyofahamu tutakuwa na mkutano mkubwa uaaohusiana na masuala ya nishati lakini tumeshuhudia nchi yetu ikipokea wageni wengi na hasa viongozi wakubwaa kutoka katika nchi mbalimbali barani Afrika pamoja na Taasisi zinazojihusisha na masuala ya Nishati”, amesema Mhagama.

Ameongeza,”Tumejiandaa na kuchukua tahadhari ya kutoa matibabu ya aina yoyote kwa jambo lolote ambalo litatokea kipindi hiki mkutano utakapokuwa ukiendelea hivyo leo nikiwa nimeambatana na Katibu Mkuu na baadhi ya viongozi kutoka kwenye taasisi za tiba nchini imetupasa kuja kukagua taasisi moja badaa ya nyingine na kujihakikishia kama maandalizi yetu yapo tayari kuwapokea wageni tumeanza hapa Agha Khan kwa kweli niwahakikishie wapo tayari tena katika viwango vya hali ya juu,”

Mganga Mkuu wa Taasisi ya Afya ya Agha Khan Dk. Harrison Chuwa

Mhagama amesema kuwa Hospitali ya Agha Khan imekamilika kwenye huduma za matibabu kila idira “Tumekagua emergency kwa kweli eneo la dharula liko vizuri , ICU maeneo ya vifaa tiba yako vizuri kila kitu kipo vizuri “.

Waziri amesema kuwa Serikali ya Tanzania itautumia mkutano huo kutangaza utalii wa tiba.

Mganga Mkuu wa Taasisi ya Afya ya Agha Khan Dk. Harrison Chuwa amesema kuwa Hospitali yao imejiandaa kwa ajili ya kutoa huduma kwa viongozi waliohudhuria mkutano wa Nishati safi Afrika.

“Tumejiandaa kwa ajili kuwahudumia wageni wetu sisi tumepokea kwa mikono miwili jukumu la kuwa moja ya hospitali itakayowahudimia viongozi waadhamizi waliohudhuria Mkutano mkuu wa Nishati”, amesema Chuwa

Dk. Chuwa amesema kuwa serikali imejiridhisha kuwa hospitali hiyo inastahili kuwahudumia wageni hao wenye hadhi.

About The Author

error: Content is protected !!