KISHINDO cha Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (MSLAC) kimeanza leo katika mikoa sita ikiwamo Kigoma huku jamii imetakiwa kutumia fursa hiyo ili kupata ufumbuzi changamoto za kisheria zinazowakabili ikiwamo migogoro ya ardhi, ndoa, mirathi, ukatili wa kijinsia na wosia. Anaripoti Danson Kaijage, Kigoma … (endelea).
Aidha, kampeni hiyo imeanza leo tarehe 23 Januari 2025 kwa kuwajengea uwezo watoa huduma za msaada wa kisheria kwenye halmashauri zote za Mkoa wa Kigoma ili kutoa huduma bora kwa wananchi.
Akifungua mafunzo ya wataalamu watakaoshiriki katika utoaji wa huduma ya msaada wa kisheria katika halmashauri za Mkoa wa Kigoma jana, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Thobias Andengenye ameipongeza Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kila Mwananchi anapata Haki na kwa wakati kupitia Kampeni ya Msaada wa Kisheria.
Amesema kampeni hiyo imelenga kutoa fursa ya kufikisha huduma ya utoaji haki za kisheria kwa wahitaji ambao wameshindwa kuzifikia huduma hizo kwa kukosa uelewa wa kisheria au kunyimwa haki zao.
Ameeleza kuwa suala la kupata haki ni msingi wa kila binadamu hivyo serikali imedhamiria kufanya kazi kwa karibu na jamii ili kuhakikisha kila mtu anapatiwa haki yake kupitia huduma ya msaada wa kisheria.
Amewasisitiza wataalamu hao kwenda kutoa elimu na msaada wa kisheria katika masuala yanayohusu ndoa, ukatili wa kijinsia, ardhi, mirathi, madai, jinai, haki za binadamu na utawala bora.
ZINAZOFANANA
TMA yatoa utabiri wa msimu wa mvua za masika 2025
Majaliwa: Serikali imefanya uwekezaji mkubwa kwa TMA
Waziri Jafo akagua maandalizi miaka 60 ya CBE