MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), kupitia serikali imedhamilia kuboresha mfumo wa utoaji wa vitambulisho hivyo, ambapo hivi karibuni wanatarajia kutoa vitambulisho zaidi ya 400,000 ambavyo vitatolewa kwa siku. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea)
Kwa sasa, NIDA imeboresha uwezo wake wa kutengeneza na kutoa vitambulisho, hili ni ongezeko kubwa ikilinganishwa na miaka ya nyuma, na ni matokeo ya juhudi za serikali kuboresha miundombinu ya teknolojia, kuongeza watumishi wenye ujuzi, na kuondoa changamoto zilizokuwa zinakwamisha mchakato huo.
Moja ya faida za ufanisi huo ni Kukuza Haki za Kiraia, kwa Wananchi wengi zaidi sasa wanapata Vitambulisho vya Taifa kwa wakati, jambo linalorahisisha upatikanaji wa huduma mbalimbali kama benki, afya, na elimu.
Pili Kuimarisha Takwimu za Kiserikali, kwani vitambulisho vinasaidia katika ukusanyaji wa takwimu sahihi kwa ajili ya mipango ya maendeleo.
Tatu Kukuza Uchumi, kwa kuwa mfumo huu unarahisisha ushirikishwaji wa wananchi kwenye shughuli za kiuchumi na huduma za kifedha.
Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza mara kwa mara umuhimu wa kuwatumikia wananchi kwa ufanisi na weledi. Mafanikio haya ya NIDA ni uthibitisho wa dhamira hiyo, na ni hatua nyingine muhimu katika safari ya kuijenga Tanzania mpya yenye maendeleo na ustawi kwa wote.
Serikali itaendelea kuboresha huduma za utoaji wa Vitambulisho vya Taifa ili kuhakikisha kila Mtanzania anapata haki yake kwa wakati. Hongera NIDA, na hongera kwa Serikali ya Awamu ya Sita!
ZINAZOFANANA
Maria Sarungi apatikana akiwa hai
Maria Sarungi atekwa nchini Kenya
Serikali yasisitiza umuhimu wa mafunzo ya ufuatiliaji miradi yake