MWANACHAMA wa Chama Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Godlisten Malisa ametahadharisha chama chake kufanya uchaguzi wa ndani na kueleza kufanya hivyo ni makosa ya kikamkati. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Hayo ameyasema leo tarehe 12 Januari 2025 alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari juu ya Tathimini yake ya uchaguzi wa chama hicho.
Amesema kuwa aliwahi kumshauri Katibu Mkuu wa zamani Dk. Vicent Mashinji kuwa uchaguzi ukifanyika karibu na uchaguzi ni makosa kimkati kwa sababu watatumia muda mchache kuyatibu majeraha ya ndani kisha kuingia kwenye uchaguzi Mkuu.
“Huenda tukaenda kwenye uchaguzi mkuu tukiwa hatupo pamoja na pia tunaweza kuwapa nafasi wale waliojeruhiwa kwenye uchaguzi kuhamia kwenye vyama vingine” amesema Malisa.
Malisa amesema kuwa uchaguzi huo ukiisha kutabakia miezi mitano ya maandalizi wa uchaguzi kipindi ambacho chama hakitapata muda mzuri wa kujiandaa na uchaguzi.
Malisa amesema kuwa chama hicho kitapata wakati mgumu kukiunga Chadema wakati kimepita kwenye mpasuko wa uchaguzi.
Malisa ataja mambo sita kuiponya Chadema, mosi, Sekretariati iwakumbushe wagombea kanuni za uchaguzi zinazuia wagombea na wapambe wao kutoa lugha chafu “ni album viongozi wanawadhalilisha viongozi wenzao na wamelala na Katiba” .
Pili, Hatua za kinidhamu zichukuliwe kama uongozi wa Kanda ya Serengeti dhidi ya Mwenyekiti wa Mkoa wa Shinyanga. Tatu wagombea na wapambe wao wakumbuke huu ni uchaguzi ndani ya chama sio vita wanaweza kushinda bila kukashifiana.
Nne, Uchaguzi wa ndani ufanyike baada ya uchaguzi Mkuu ili kuondoa nafasi ya watu wanaoweza kukimbia chama wakihisi wameonewa, na kwamba muda huo ni mfupi wa kutiba majeraha .
Tano, Kuundwe kamati Maalum ya kutibu majeraha yaliyotokana na kampeni hizi na hapa tunaweza kuwatumia viongozi wa dini na wazee wa chama. Sita, wagombea washikane mikono na wakubaliane ili kuondoa mpasuko utakaosababishwa na uchaguzi
ZINAZOFANANA
Dk. Slaa aburuzwa kortini apelekwa lupango
JOkate awapa tano vijana kwa maandalizi ya Mkutano Mkuu wa CCM
Dk Slaa akamatwa usiku ‘mnene’ Dar