January 10, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Dk. Slaa aburuzwa kortini apelekwa lupango

Dk. Wilbroad Slaa

 

ALIYEKUWA balozi Tanzania nchini Sweden, Dk. Wilbord Slaa ameshtakiwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kwa tuhuma za kuchapisha taarifa za upongozi kwenye mtandao wa X. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

DK. Slaa aliyepandishwa kizambani leo tarehe 10 Januari, 2025 amesomewa shtaka moja kwenye kesi Na.993 ya mwaka 2025 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Beda Nyaki na kunyimwa dhamana baada ya mawakili wa Jamhuri kuwasilisha kiapo cha kupinga mwanasiasa huyo asipewe dhamana kwa kile walichodai usalama wake utakuwa shakani.

Dk. Slaa anatuhumiwa kusambaza maneno ya uongo kwa kuandika kwenye ukurasa wa mtandao wa X’ kwamba kuna mawasiliano kati ya Rais na Mwamba kuhusu kupeana msaada wa kifedha.

Wakili Boniface akizungumza na waandishi wa habari mahakamani hapo, Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika, Boniface Mwabukusi, amedai kuwa mawakili wa Jamhuri wameshtukiza ombi la kunyimwa dhamana kwa Dk. Slaa hivyo kumfanya mwanasiasa huyo kwenda rumande mpaka Jumatatu, tarehe 13 Januari 2025 kwa ajili ya usikilizaji wa pingamizi hilo.

“Dhamana ni haki ya mtuhumiwa huwezi kumnyima mtu dhamana kwa kauli ya ujumla na sheria ni uwanja unaohitaji uadilifu sio kushtukiza kama tulivyoona leo, watu wamekuja na viapo wameficha kwapani jambo ambalo wangewapa mapema mawakili wa upande wa pili wangeweza kujiandaa kwa majibu ya hoja ili Mahakama iamue,” amedai Mwabukusi.

About The Author

error: Content is protected !!