KADA wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), na Mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Shinyanga Emmanuel Ntobi avuliwa uanachama wake kwa madai ya utovu wa nidhamu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Shinyanga … (endelea).
Katibu wa Chadema Kanda ya Serengeti Jackson Mnyawami amesema kuwa kikao cha Kamati tendaji Kanda ya Serengeti imemvua Ntobi uongozi kwa makosa ya kukiuka maadili na utovu wa nidhamu ikiwemo kuchafua viongozi wa chama hicho kupitia mitandao ya kijamii.
Ntobi mwenyewe amekiri kuvuliwa uongozi lakini ameonewa na kwamba hakupewa nafasi ya kusikilizwa.
“Nimeonewa kwa sababu nilitakiwa kufikishwa kwenye kamati ya nidhamu ili nisikilizwe lakini bahati mbaya kamati ilikaa na kufanya uamuzi bila kunisikiliza , wakili wangu anashughulikia rufaa juu ya suala hilo”
Mwenyekiti wa Kanda ya Serengeti Lucy’s Ngoto amesema kuwa Ntobi alipewa nafasi ya kujitetea sio kweli kwamba hakusikiizwa kama anavyodai
ZINAZOFANANA
Viongozi CWT lawamani kwa matumizi mabaya, kutowalipa wastaafu
Makala apata kigugumizi kinachoendelea Chadema
Mvua zakatisha mawasiliano kwa wananchi wa Ulanga