January 8, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

CHAKUHAWATA yafanya mkutano wa kurekebisha Rasimu ya Katiba

 

WAKATI chama cha Walimu Tanzania CWT wakijiandaa na chaguzi zao kuanzia ngazi ya matawi hadi taifa chama cha kulinda na kutetea haki za walimu Tanzania (CHAKUHAWATA) nao wamefanya mkutano wao maalumu wa marekebisho ya Rasimu ya katiba yao. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Mkutano huo uliofanyika Jijini Dodoma ulikuwa na ulinzi mkali kutoka kwa Jeshi la polisi waliovalia sale za jeshi hilo na waliokuwa wamevaa kirahia na kutapakaa kila sehemu za maeneo ya ukumbi wa mikutano.

Hali ya kuimarisha ulinzi kwa kutumia polisi wengi waliovalia sale za kazi na wengine kuvaa kiraia inatafsiriwa kuwa ni hatua ya kujiami na fuzo zinazoweza kujitokeza kutokana na baadhi ya viongozi na walimu kutounga mkono uanzishwaji wa chama hicho.

Chakuhawata ni chama cha kulinda na kutetea haki za walimu Tanzania ambacho kilijimega kutoka kwenye chama cha walimu Tanzania (CWT) Kutokana na kuwepo kwa migogoro mbalimbali ya CWT kutokana na uongozi uliopo sasa kushindwa kusimamia katiba na kutetea masilahi yao hususani kushindwa kuzungumzia makato ya asilimia mbili .

Katibu wa CHAKUHAWATA Mkoa wa Tanga na mjumbe wa Mkutano Mkuu Saimoni Antony amesema kuwa uanzishwaji wa chama hicho kilichoanzishwa toka mwaka 2015 kimekuwa na manufaa makubwa kwa wanachama kwani chama hicho kwa ajili ya kutatua migogoro,haki na kutatua migogoro kwa wanachama tofauti na kilivyo chama cha wezao walimu.

Antony amesema kuwa mkutano mkuu huo umekaa kwa ajili ya kufanya marekebisho ya rasmi ya katiba pendelezwa ambayo itakuwa dira na mwongozo wa walimu na kuwafanya kuachana na michango mikubwa wanayokatwa walimu.

Chama hicho chenye makao makuu yake Kigoma kimenzishwa takribani miaka 10 sasa na kinaendelea kuboresha rasimu ya katiba yao yenye kurasa 54 ambayo ikisha kuwa tayari watapitisha na kanuni zao.

Hata hivyo wajumbe wa mkutano huo wamewataka waajiri hususani kwa ngazi ya wilaya kuwaruhusu walimu kujiunga katika chama hicho kadri mwalimu atakavyopendezwa badala ya kuwalazimisha kujiunga katika vyamaba ambavyo mwalimu hapendezwi navyo.

About The Author

error: Content is protected !!