MSANII wa Bongo Fleva, Rajab Abdul ‘Harmonize’ ameshirikishwa na staa wa muziki kutoka nchini Ghana, KJ Spio katika kibao kiitwacho ‘Messi”. Anaripoti Joseph Shaluwa, Dar es Salaam … (endelea).
Katika kolabo hiyo, mbali na Harmonize, KJ amemshirikisha mwanamuziki mwingine, mkali wa Dancehall kutoka Jamaica, Konshens ambao kwa pamoja wamenogesha singo hiyo.
Ngoma hiyo ambayo imetayarishwa na mshindi wa Tuzo ya Grammy, Mjamaika Izzy Beats, aliyefanya pia kazi za wakali kamaJorja Smith, Rema, Koffee, Masego, Alicia Keys na wengineo, ina mikito ya Afrobeats, Dancehall na Amapiano.
Mchanyato wa wasanii hao, KJ Spio, Harmonize na Konshens, unajifanya ngoma hiyo kuwa ya aina yake na isiyochosha masikioni mwa msikilizaji.
Akizungumzia wimbo huo, KJ Spio anasema: “Mimi ni shabiki mkubwa wa Konshens, na baada ya kufanya kazi na Harmonize awali, niligundua kwa pamoja tunaweza kufanya kitu kizuri. Kwa hiyo nikachukua uamuzi huo na kilichotokea kinakwenda kutengeneza historia.”
Harmonize naye akizungumzia ushiriki wake katika singo hiyo alisema: “Huu wimbo ni mzuri sana kuwahi kutokea. Ni muziki wa kimataifa, utasumbua sana ndani na nje ya bara letu la Afrika.”
Konshens akasema: “Kufanya kazi na Harmonize na KJ Spio ni ushiriki mzuri, tulipata muda mzuri wa kuandika, kukagua ala za muziki na hatimaye kurekodi video. Ninapenda sana muziki kutoka kwetu. Ni kazi nzuri sana kwa hakika.”
ZINAZOFANANA
Moto wa Chelsea waendelea kuwaka huko Uingereza
Tusua na wakali wa ubashiri Jumapili ya leo
Bruce Melodie adondosha “Niki Minaji” X Blaq Diamond