WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo amesema pamoja na mambo mengine, dira mpya ya maendeleo ya Taifa ya mwaka 2050 utaijenga Tanzania kuwa Taifa jumuishi lenye ustawi, haki na linalojitegemea. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).
Katika kufikia huko, Waziri Kitila wakati wakati wa Uzinduzi wa Rasimu ya Kwanza ya Dira 2050, amewaambia wanahabari kuwa kufikia mwaka 2050, Tanzania inatakiwa kuwa imeingia kwenye nchi za Kipato cha Kati ngazi ya juu ikichagizwa na sekta ya uzalishaji viwandani, ili kufikia pato la mtu mmoja la Dola za Marekani 4700 huku pato la Taifa likitarajiwa kufikia Dola za Marekani Bilioni 700.
Aidha kulingana na Waziri Kitila Mbele ya Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Mwinyi na Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, Dira 2050 imenuia pia kuondoa umaskini uliokithiri na kupunguza umaskini wa mahitaji ili kuwa chini ya asilimia 5 kutoka asilimua 26 ya hivi sasa.
Katika hatua nyingine akieleza shabaha nyingine ya Dira 2050, Prof. Kitila Mkumbo amesema Tanzania imedhamiria kuwa kinara wa uzalishaji wa Chakula barani Afrika pamoja na kuwa wazalishaji wakubwa kumi wa Chakula duniani.
Shabaha nyingine ya Dira 2050 ni pamoja na kuifanya lugha ya kiswahili kuwa lugha inayoheshimika na kuwa kati ya lugha mbili kubwa barani Afrika na lugha rasmi kwenye Vikao na shughuli za Umoja wa Mataifa.
Tanzania pia imenuia kuwa Taifa linalojitegemea katika mahitaji ya umeme ambapo wastani kwa mtu mmoja yatakuwa Kilowati 600 kufikia mwaka 2050 kutoka Kilowati 200 za hivi sasa. Kadhalika kufikia 2050 Dira 2050 inataka kila Mtanzania kuwa na elimu ya kidato cha nne na asilimia 15 wawe na elimu ya ngazi ya juu yenye ujuzi stahiki na shindani kwenye soko.
ZINAZOFANANA
Mwabukusi: Chadema tutawaadhibu, msipowasiliza wananchi
Mbowe, Lissu wawagawa viongozi wa Kigoma
Rais Samia kwenda na Dk. Nchimbi 2025