KAMBI Tiba ya Madaktari Bingwa kutoka Tanzania nchini Comoro imeanza kwa mwitikio mkubwa wa wananchi wa nchini humo ambapo mamia wamejitokeza kupata huduma mbali mbali zinazotolewa kwa ushirikiano na madakatari wazawa katika Kisiwa cha Ngazidja. Anaripoti Mwandishi Wetu, Comoro … (endelea).
Madaktari hao wa Tanzani wametoa huduma za uchunguzi na matibabu katika matatizo ya mifupa,figo na kibofu cha mkojo, mifupa, saratani, moyo na mengineyo ambapo takriban wagonjwa 417 wameandikishwa katika siku ya kwanza.
Akizungumza katika kikao cha tathmini ya uendeshaji wa kambi hiyo inayoratibiwa Ubalozi wa Tanzania nchini Comoro na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Kaimu Mkuu wa Msafara, Dk Salehe Mwinchete alieleza kuwa ushirikiano waliopewa na madaktari wenyeji ni mkubwa na wananchi wa Comoro wamejitokeza kwa wingi na hilo limewatia moyo kuwa siku zinazofuata hali itakuwa bora zaidi.
Naye Balozi wa Tanzania nchini Comoro aliwaaeleza madaktari hao kuwa Kambi Tiba hiyo imekuwa kivutio kikubwa na wananchi wengi wana imani kuwa katika Kambi zijazo fani nyingine za afya zitaingizwa.
Kambi hiyo itakayohitimishwa tarehe 4 Desemba,2024,inashirikisha madaktari bingwa kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Hospitali za Benjamin Mkapa, Hospitali ya Muhimbili, Taasisi ya Saratani ya Ocean Road na Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (MOI).
ZINAZOFANANA
Wasanii wamiminika JKCI ofa ya Rais Samia kupima moyo
Morocco kuwapa wanawake haki zaidi
Wakazi wa Mdundwaro waishukuru TASAF kuwajengea nyumba ya watumishi