CHAMA cha upinzani nchini Namibia kimeomba zoezi la kuhesabu kura lisitishwe baada ya uchaguzi wa taifa kukabiliwa na changamoto za kiufundi huju upigaji kura ukiendelea baada ya muda wa kufungwa kwa vituo vya kupigia kura. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).
Uchaguzi wa rais na bunge ni mtihani mkubwa kwa chama tawala cha SWAPO ambacho kimetawala katika taifa hilo lenye utajiri wa madini tangu lijipatie uhuru miaka 34 iliyopita na kinakabiliwa na uchaguzi wenye upinzani mkali.
Baadhi ya wapiga kura walikuwa kwenye foleni usiku Jumatano baada ya mamlaka kuruhusu vituo vya kupigia kura kufunguliwa baada ya muda uliopangwa wa kuvifunga saa tatu usiku kutokana na kuwa watu wengi sana walikuwa bado wakisubiri kupiga kura.
Baadhi ya vituo vya kupigia kura vilianza hata hivyo kuhesabu kura.
“Kuna vituo vya kupigia kura ambavyo vimeanza kutangaza matokeo, kuna vituo vya kupigia kura ambavyo vinatwambia viliamrishwa kusitisha zoezi la kuhesabu kura,” alisema Christine Aoachamus kutoka chama kikuu cha upinzani, Independent Patriots for Change(IPC) Alhamisi.
ZINAZOFANANA
Lungu akwama kuwania urais Zambia
Wananchi Comoro wafurahia huduma madaktari wakitanzania
Ushiriki wa Rais Samia G20 wainufaisha Tanzania