November 25, 2024

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Wawekezaji biashara ya kaboni watakiwa kuwa wawazi

 

SERIKALI ya Tanzania imetoa wito kwa kampuni zinazojihusisha na biashara ya kaboni nchini kujenga uwazi na kuhusisha jamii kwenye maeneo ya miradi ili wananchi wawe nba ufahamu wa biashara hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Baku, Azerbaijan … (endelea).

Pia, imezitaka kampuni hizo kutimiza ahadi wanazoweka katika biashara ya kaboni ili kuleta manufaa ya kuhifadhi bionuwai na faida kwa jamii.

Wito huo umetolewa na Mhifadhi Mkuu kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Dk. Elikana John aliposhiriki mkutano wa pembezoni wakati wa Mkutano wa 29 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP29) jijini Baku, Azerbaijan.

Mkutano huo umeandaliwa na Kampuni ya Terraformation wenye mada iliyolenga upatikanaji wa fedha kwa ajili ya uongoaji wa ardhi na misitu kupitia biashara ya kaboni.

Katika majadiliano hayo, Dk. Elikana alieleza kwa kampuni hiyo kuwa nchi imeweka lengo la kurudishia hekta milioni 5.2. ilikratibiwa na TFS na Ofisi ya Makamu Rais.

Ameongeza kuwa pamoja na mambo mbalimbali tayari Ofisi ya Makamu wa Rais imeshaandaa Kanuni na Mwongozo wa biashara hiyo ili iweze kuinufaisha jamii.

Ili kufanikisha hayo, Dk. Elikana aliongezea kwa kusema kuwa Tanzania inahitaji uwekezaji na ufadhili wa miradi hiyo kutoka kwa wadau mbalimbali duniani kote.

Halikadhalika, amebainisha kuwa utalaam wa kuandaa miradi hiyo unahitajikapamoja na kufanyika kwa tafiti kwenye maeneo ya misitu ili kuja na matokeo chanya.

About The Author