KATIBU wa Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Itikadi, Uenezi,Siasa na Mafunzo, Amos Makala amesema amemsikia Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe Akieleza kuwa Chama chake hakina Ilani na wagombea wao watatakiwa kubuni buni Ilani tu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Makala ameyasema jana tarehe 20 Novemba 2024 mbele ya wananchi wakiwemo wana CCM wilayani Temeke mkoani Dar es Salaam alipokuwa akizindua kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa,vijiji na vitongoji unaotarajia utafanyika tarehe 27 Novemba 2024.
Akizungumza mbele ya mamia ya wananchi hao Makala amesema amefuatilia hotuba ya Mbowe jana na amemsikia akisema Chama chake hakina Ilani na ameagiza kila mgombea atakayeteuliwa katika Kijiji chake au katika mtaa wake abuni Ilani yake “Nilisikia hivyo kwamba wao hahawawezi kuandika Ilani, hawana jambo lolote la kusimamia uchaguzi huu ila wamewaagiza wagombea wao kubuni buni Ilani ya mtaa au kama kuna kijiji abuni yeye Ilani ya pale.
“Kwahiyo mnaweza kupata picha mnaenda katika uchaguzi kuna Chama kimeleta maendeleo na mafanikio, kuna chama kina Ilani lakini kuna chama kingine kinakuja kuomba kura lakini kinawathabitishia Watanzania kwamba wao hawakujipanga na wanataka wagombea wao wabuni Ilani katika kijiji anachokaa”
“Pamoja na Ilani sisi Chama Cha Mapinduzi tumetoa tamko la kusimamia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa,hawa wagombea wetu watakuwa wanajinadi lakini watakuwa wanatumia tamko la Chama Cha Mapinduzi.”
ZINAZOFANANA
Ushindi wa Profesa Lipumba wapingwa
Sativa amlipia Lissu fomu ya kugombea Uenyekiti Chadema
John Tendwa afariki dunia